Msanii wa Bongo flava na mfalme wa miduara AT, akiongelea utamaduni wa kiswahili na raha za pwani kwenye jopo la kongamano la raha za pwani kwa lengo la kudumisha na kutangaza utamaduni wa Mswahili na lugha yake.na baadae kuonesha onesho kali ya nyimbo zake zilizotamba na zinazoendelea kutamba kwenye anga ya bongo na kimataifa. Kongamano hilo linaloambatana na tamasha la Mswahili na lugha yake huandaliwa na Swahili Media Network na hufanyika mara moja kila mwezi. Picha na Vijimambo Blog na Kwanza Production.
Msanii wa Bongo flava mfalme wa miduara AT akichengua mashabiki wake kwa wimbo mmoja wapo wa mduara.
Msanii wa Bongo flava mfalme wa miduara AT usipime ni balaa
Msanii wa Bongo Flava Mr. Tz akitoa buradani kwenye jopo la kongamano la raha za pwani lililofanyika siku ya Jumamosi July 22, 2017 Hampton Inn, College Park, Maryland.
Msanii wa Bongo Flava Mr. Tz akitoa buradani kwenye jopo la kongamano la raha za pwani
Aisha akifungua pazia kwenye jopo la kongamano la raha za pwani kwa lengo la kudumisha na kutangaza utamaduni wa Mswahili na lugha yake.na baadae kumkaribisha mratibu wake Bwn. Mgaza (hayupo pichani).
Mratibu wa Raha za Pwani Bwn. Mgaza akiuelezea Utamaduni wa Kiswahili na lugha yake kwenye jopo la kongamano la raha za pwani lililofanyika siku ya Jumamosi July 22, 2017 College Park, Maryland.
Bi Rukia akichangia nini maana ya Utamaduni wa Kiswahili na lugha yake kwenye jopo la kongamano la raha za pwani lililofanyika siku ya Jumamosi July 22, 2017 College Park, Maryland na huku akitoa rai kwa wazazi ughaibuni kuacha kudharau utamaduni wa wetu na wafanye kazi ya ziada kuwafundisha watoto wa ughaibuni lugha ya Kiswahili na utamaduni wake.
Mama mitindo na mkurugenzi wa Miss Tanzania USA MaWiny Casey akichangia vazi la khanga na utamaduni wa Kiswahili na lugha yake kwenye jopo la kongamano la raha za pwani lililofanyika siku ya Jumamosi July 22, 2017 College Park, Maryland.
Mama mitindo na mkurugenzi wa Miss Tanzania USA MaWiny Casey akimkabidhi tuzo Mwenyekiti Mtendaji wa Baraza linalosimamia shughuli za utamaduni na Sanaa nchini Tanzania (BASATA) - Bwana GODFREY LEBEJO MNGEREZA, aliefuatana na Msanii maarufu wa nyimbo na ngoma ya Muduara- Bwana ALI RAMADHAN ALI, al-maarufu kwa jina la MR. AT kwenye jopo la kongamano la raha za pwani lililofanyika siku ya Jumamosi July 22, 2017 College Park, Maryland.
Mwenyekiti Mtendaji wa Baraza linalosimamia shughuli za utamaduni na Sanaa nchini Tanzania (BASATA) - Bwana GODFREY LEBEJO MNGEREZA akiongelea muziki unavyodumisha utamaduni wa Kiswahili na lugha yake kwenye jopo la kongamano la raha za pwani lililofanyika siku ya Jumamosi July 22, 2017 College Park, Maryland.
Watoto Imani (kushoto)naAaliyah wakicheza moja ya mchezo ya watoto wanavyocheza kwa Kiswahili kama moja ya kudumisha Kiswahili na utamaduni wake.
Kwa picha zaidi bofya soma zaidi
No comments:
Post a Comment