ANGALIA LIVE NEWS

Monday, September 11, 2017

Dc’s na Ded’s wabebeshwa mzigo mzito

 Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe Selemani Jafo akizungumza  katika hafla ya kufungua mafunzo ya Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi  katika Ukumbi wa Hazina Mjini Dodoma leo.
 Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia Afya Dkt. Zainabu Chaula akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi, Prof. Joseph Semboja  akiwasilisha taarifa ya awali kwa Mgeni Rasmi na Washirki wakati wa  kufungua mafunzo ya Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi  katika Ukumbi wa Hazina Mjini Dodoma leo.
 Baadhi wa wa Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa walioshiriki kwenye mafunzo ya uongozi yanayoendeshwa na Ofisi ya Rais Tamisemi kwa ushirikiano na Taasisi ya Uongozi.
Naibu Waziri wa OR-Tamisemi Mhe. Selemani Jafo (mbele katikati), akiwa kwenye picha ya pamoja na Naibu Katibu Mkuu Tamisemi Dkt. Zainabu Chaula (mbele kushoto), Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Uongozi Prof. Joseph Semboja (mbele kulia) pamoja na baadhi wa wafanyakazi wa Taasisi ya Uongozi walioandaa mafuno haya.

Nteghenjwa Hosseah, Tamisemi – Dodoma.
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala  za Mikoa  na Serikali za Mitaa  Mhe. Selemani Jafo amewataka Wakuu wa Wilaya  na Wakurugenzi wote nchini kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi  ili kutimiza matarajio  ya watanzania  ambao wanaitegemea Wizara hii kama chachu ya  mabadiliko  katika utendaji kazi wa Serikali ya awamu ya Tano. 
Mhe.Jafo ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri za Mikoa ya Dar es Salaam, Shinyanga, Mbeya, Songwe, Rukwa, Ruvuma, Iringa na Njombe yanayoendeshwa na Ofisi ya Rais Tamisemi kwa ushirikiano na Taasisi ya Uongozi.
Akiungumza katika ufunguzi wa mafunzo hayo  Mhe.Jafo amewataka viongozi hao kutumikia Wananchi kwa kuzingatia Taratibu, Sheria na Kanuni za Utumishi wa Umma huku wakizingatia mipaka yao ya Utawala, kuboresha mahusiano katika maeneo ya kazi na  kuhakikisha hakuna muingiliano wa majukumu baina ya viongozi wa Wilaya na Halmashauri. 
“Nafahamu baadhi viongozi  mlitokea katika sekta binafsi na humkuwa mnafahamu vizuri utendaji kazi wa shughuli za Serikali hata hivyo mmefanikiwa  kwa kipindi chote kutenda kwa kadiri ya maelekezo ya Serikali,vipaumbele na miongozo mbalimbali  iliyotolewa pia mmejitahidi kutoa huduma bora ukiachilia mbali mapungufu madogo madogo ambayo tumeyabaina na kuyashuhudia katika baadhi ya maeneo” alisema Jafo.
Aliongeza kuwa “kupitia mafunzo haya ni imani yangu kuwa wote sasa tutakuwa na uelewa wa pamoja wa kufanya kazi Kimkakati ili kuwaletea wananchi maendeleo huku mkifahamu vyema Muundo wa Serikali na namna inavyofanya kazi kwa kuzingatia mipaka na mgawanyo wa majukumu, Itifaki, utunzaji wa Siri za Serikali na maadili ya viongozi wa Umma”.
Aidha Mhe. Jafo aliwataka viongozi hao kuendelea kusimamia nidhamu ya watumishi, kuendeleza mapambano dhidi ya Dawa la kulevya, kulinda amani na utulivu katika maeneo yao huku  wakisimamia kwa makini mapato na matumizi ya Fedha za Serikali na kusisitiza matumizi ya mifumo ya Kielektroniki katika ukusanyaji wa mapato ya Serikali.
Akimkaribisha Mgeni rasmi katika mafunzo hayo Naibu Katibu Tamisemi anayeshughulikia Afya Dkt. Zainabu Chaula amesema kitu cha msingi kati yetu sisi watendaji ni umoja ambao kupitia huo  utatuleta Ushindi  na muongozo wa utendaji wetu uko kwenye ilani ya Chama cha Mapindui hivyo kila mmoja wetu arejee Ilani ile ili afahamu nini anachotakiwa kukifanya katika kipindi hiki cha miaka mitano.
Awali akitoa taarifa  ya utangulizi kwa mgeni rasmi na washiriki wa mafunzo hayo Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi Prof. Joseph Semboja alisema  mafunzo haya yanatolewa na wataalamu walioboea katika masuala ya uongozi na yatafanyika kwa muda wa siku tano kwa viongozi aidi ya 72.
Aliongeza kuwa maeneo ambayo yatajen gewa uwezo ni namna bora ya  kufanya maamuzi ya kimkakati yanayozingatia mahitaji na manufaa mapana ya Taifa, namna bora ya kuongoza watu na kusimamia Rasilimali za Taifa na pia  jinsi ya  kujijengea Sifa za kiungozi ambazo zinaleta heshima kwa jamii, kuaminika na kutegemwa katika kuleta mabadiliko.
Mafunzo haya yamepangwa kufanyika katika awamu nne(4) ambapo awamu mbili tayari zimekwsihafanyika ziliojumuisha Wah. Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi kutoka Mikoa kumi na mbili(12) ya Dodoma, Morogoro, Singida, Tabora, Kigoma, Katavi, Kagera, Mwana, Mara, Simiyu, Geita na Manyara.
Awamu ya kwanzaya mafunzo haya ya Uongozi  yalifanyika Mwezi Mei, 2017 na  yalifunguliwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa na awamu ya mwisho inatarajiwa kufanyika kabla ya mwezi Disemba 2017.

No comments: