ANGALIA LIVE NEWS

Friday, September 29, 2017

Madiwani wawili Chadema washikiliwa polisi

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Mathias Nyange.

By Stephano Simbeye, Mwananchi ssimbeye@mwananchi.co.tz

Madiwani wawili wa Chadema EmmanuelMwalupasa na Jailo Mwandute katika Halmashauri ya Mji wa Tunduma wilayani Momba wanashikiliwa na polisi wakituhumiwa kwa makosa tofauti ya jinai.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Mathias Nyange amesema Mwalupasa ambaye ni diwani wa Mpande anatuhumiwa kufunga ofisi ya mtendaji kata kwa siku tatu mfululizo.

Kuhusu diwani Mwandute wa Kata ya Katete, amesema anatuhumiwa kwa wizi wa zaidi ya Sh10 milioni ambazo ni kwa ajili ya maendeleo ya kata hiyo.

Kamanda Nyange amesema madiwani hao walikamatwa jana Alhamisi jioni na kufikishwa kituo kikuu cha polisi mjini Tunduma ambako wanaendelea kushikiliwa.

Amesema wanaendelea na uchunguzi kuhusu tuhuma zinazowakabili madiwani hao.

No comments: