Chamwino. Mikoa minne imetajwa kuwa kinara katika mimba za utotoni hali inayoonyesha bado kuna tatizo.
Ofisa maendeleo ya jamii wa Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma, Sophia Swai amesema hayo alipozungumzia suala la mimba shuleni.
Swai ameitaja mikoa ambayo ni vinara wa mimba za utotoni na asilimia zake zikiwa kwenye mabano kuwa ni Shinyanga (59), Tabora (58), Mara (55) na Dodoma (51).
Amesema taarifa ya mwaka 2011 inaonyesha hali ya mimba za utotoni bado ni janga linalotakiwa kushughulikiwa na wadau wote.
Swai ameagiza jamii kubadilika na kuacha mila potofu kwa kuwa hali kwa sasa inahitaji watu wote kusoma na kuwa na haki sawa.
No comments:
Post a Comment