Kikao cha Baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Handeni nusura kivunjike baada ya kuibuka hoja inayohusu kujengwa kwa makao makuu ya wilaya kati ya mji mdogo wa Mkata au Kabuku hali ambayo ilibidi busara zitumike ili kikao kiendelee.
Hoja hiyo ambayo iliwasilishwa na diwani wa kata ya Mkata Mh Musa Mwanyumbu huku akimtuhumu Mwenyekiti wa halmashauri hiyo kuwa anapendelea upande mmoja.
Kufuatia hatua hiyo baadhi ya madiwani wameomba kama kuna vyombo vya juu vinavyohusika na jambo hilikufika ili kuliweka sawa jambo hili.
Chanzo: ITV Tanzania
No comments:
Post a Comment