Thursday, September 7, 2017

Updates: Tundu Lissu apigwa risasi nyumbani kwake mkoani Dodoma

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu amepigwa risasi leo Alhamisi nyumbani kwake na kwamba hali yake ni mbaya.
Lissu, ambaye ni mwanasheria mkuu wa Chadema kwa sasa amepelekwa chumba cha upasuaji katika Hospitali ya Rufaa ya Dodoma.
Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah, wabunge na viongozi wengine wa ulinzi wa Bunge wamefika katika hospitali hiyo kujua kinachoendelea.
Baadhi ya ndugu na wagonjwa wamefurika katika chumba cha upasuaji cha hospitali ya mkoa wakitafakari, huku wengine wakilia.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Charles Kihologwe amewataka watu hao kukaa mbali na chumba cha upasuaji lakini wengi wanakataa wakisema hawamwamini mtu yeyote.
Asubuhi, Lissu alihudhuria kikao cha Bunge na aliomba mwongozo wa Naibu Spika akihoji kuhusu taarifa za kamati zilizoundwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai kutathmini mfumo wa uchimbaji, usimamizi, umiliki na udhibiti wa madini ya Tanzanite na almasi kuwasilishwa kwa Waziri Mkuu badala ya kujadiliwa na Bunge kwanza.

Chanzo: Mwananchi

2 comments:

Anonymous said...

Hii taarifa ya kupigwa risasi ilikuwepo tangu mchana.DJ Luke nashukuru kwa kutuhabarisha,Nilitegemea ningeona details kwenye Michuzi blog hadi jioni ndiyo naona kwenye blog hiyo. Hii habari kubwa inayohusu maisha ya mtanzania na kiongozi wa bunge na rais wa chama cha wanasheria nchini.Naomba niseme jambo moja..MICHUZI YUPO VERY BIASED ndiyo anaweza akawa mouthpiece ya CCM lakini inapokuja kwenye suala la habari za kitaifa awe na uzalendo na angalau huruma japo kidogo, habarisha bila ubaguzi wananchi wote, anakuwa mwepesi kuandika habari hasi kwa vyama vya upinzani, Kama msomaji wa blog ya MICHUZI naona wazi ushabiki kuliko habari. Vichwa vya habari vya wapinzani kunyang'anywa mashamba au kukamatwa unaweka kama breaking news kwa mbwembwe nyingi. Usilete ubaguzi nchi hii ni yetu sote atasema ni blog yake na ana haki ya kuweka anachotaka na kutoweka asichotaka lakini kwenye uhuru wa kuhabarisha hakuna ubaguzi,KU ONGEA UKWELI HIYO NDIYO UWELEDI WA UANDISHI NA UTOAJI WA HABARI wakati mwingine ukweli unauma lakini ukweli ni ukweli na historia ni historia huwezi kubadili. Haya ni mambo ya aliyekuwa mbunge ABOOD wa morogoro kukataza vyombo vyake kutangaza habari za upinzani akidhani ni kuvikomoa, Tanzania hatupo hivyo tulikubali vyama vingi tuvumilie.

Anonymous said...

Inasikitisha sana, lakini sijashangazwa, kwani tunaiga mifano ya nchi jirani za Rwanda ya Kagame na Uganda ya Museveni ambako Wanasiasa wa Upinzani wanauawa kiholela. Hao si ndiyo marafiki wakubwa?...PROVE ME WRONG! Credibility ya nchi yetu kama Taifa lenye AMANI Afrika is at stake. Naiomba Serikali ya JPM ilitazame suala hili kwa makini, maana linatia dosari na huweza likasababisha wafadhili wengi wa magharibi kuanza kusita.