ANGALIA LIVE NEWS

Monday, October 2, 2017

CATALONIA YAJITENGA NA HISPANIA

KIONGOZI wa Jimbo la Catalonia, Carles Puigdemont amesema kuwa eneo hilo lililokuwa sehemu ya nchi ya Hispania limepata haki ya kuwa huru kufuatia kura ya maoni ambayo hata hivuo imekumbwa na ghasia.

Katika matokeo ya kura ya maoni yameonesha kuwa asilimia 90 ya watu wanataka Jimbo la Catalonia lipewe uhuru na mamlaka kamili.
Aidha mpaka sasa zaidi ya watu 800 wamejeruhiwa kufuatia ghasia zilizozuka baada ya Polisi kuzuia upigwaji wa kura hiyo huku polisi wakichukua makaratasi ya kupigia kura na masanduku kutoka kwa vituo vya kupigia kura.
Wakati akihutubia kupitia televisheni, Carles Puigdemont alisema kuwa sasa mlango umefunguliwa kwa eneo hilo kutangazwa kuwa huru.

“Siku hii ya leo ya matumaini na mateso, watu wa Catalonia wameshinda haki yao ya kuwa na taifa huru kama jamhuri,” alisema Puigdemont.
“Serikali yangu kwa muda wa siku chache zinazokuja itatuma matokeo ya kura ya leo kwemda kwa bunge la Catalonia, ili ifanye kuambatana na sheria ya kura ya maoni.”

No comments: