Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza akikabidhiwa ofisi na aliyekuwa Naibu Waziri wa wizara hiyo Mhe. Anastazia Wambura leo mjini Dodoma.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akisalimiana na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (katikati) baada ya kuwasili ofisini leo mjini Dodoma. Wa kwanza kulia ni aliyekuwa Naibu Waziri wa Wizra hiyo Mhe. Anastazia Wambura.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili Ofisi za Wizara leo mjini Dodoma. Wa kwanza kushoto ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akiongea na baadhi ya viongozi na watumishi wa Wizara wakati wa kumkaribisha Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (kushoto). Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Nuru Millao.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (wa pili kushoto) akiongea na baadhi ya viongozi wa Wizara akiwemo Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (wa kwanza kushoto) mara baada ya kuwasili ofisini mjini Dodoma. Wa kwanza kulia ni aliyekuwa Naibu Waziri wizara hiyo Mhe. Anastazia Wambura.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (kushoto) akipokelewa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Nuru Millao (kulia) mara baada ya kuwasili ofisini mjini Dodoma.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza akipokelewa watumishi wa Wizara hiyo mara baada ya kuwasili ofisini mjini Dodoma.
(Picha na Eleuteri Mangi, WHUSM,Dodoma)
Na Eleuteri Mangi, WHUSM, Dodoma
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza ameahidi kushirikiana na Watendaji wa Wizara, wadau pamoja na wananchi kwa ujumla kusimamia maadili ya Mtanzania ili kuendelea kuwa na taifa bora.
Mhe. Shonza ameyasema hayo alipowasili katika ofisi za Wizara leo mjini Dodoma ambapo alipokelewa na Waziri mwenye dhamana Dkt. Harrison Mwakyembe, viongozi wa Wizara pamoja na watumishi.
“Wizara hii ni muhimu sana kwa kuwa inajenga taswira ya taifa kupitia sekta zake ambazo ni Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo hivyo ntahakikisha tunashirikiana kwa karibu katika kuwatumikia wananchi “alisema Naibu Waziri Shonza.
Aliongeza kwa kueleza kuwa atahakikisha suala la maadili bora kwa jamii linazingatiwa ili kuendelea kujenga taifa imara kwa kuzingatia mavazi yenye heshima na nyimbo zenye kujenga.
Aidha, Naibu Waziri Shonza amesema ni wajibu wetu kama watumishi wa umma kuhakikisha tunatekeleza Ilani ya chama tawala ambacho kiliahidi kuwatumikia watanzania ili kuhakikisha malengo ya Serikali yanafikiwa kwa wakati.
Naye aliyekuwa Naibu Waziri wa Wizara hiyo Anastazia Wambura amempongeza Naibu Waziri Shonza kwa kuteuliwa kushika wadhifa huo na amemshukuru Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kumuamini kuwatumikia Watanzania.
Akizungumzia utendaji kazi, Mhe. Wambura ameufananisha utumishi wa umma na chombo cha usafiri ambapo abiria hushuka kituo mara baada ya kufika na dereva kuendelea na safari.
“Mhe.Waziri, viongozi wenzangu na ndugu zangu watumishi wa Wizara, mimi nimefika kituoni, Naibu Waziri nakukabidhi kijiti endelea na safari, endelea kuwatumikia Watanzania kama ambavyo ilani ya chama tawala inavyoeleza” alisema Mhe.Wambura
Kwa upande wake Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe amemuahidi Naibu Waziri Shonza ushirikiano wa hali na mali katika kuwahudumia wananchi kupitia sekta za Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
1 comment:
Hongera sana Mheshimiwa Juliana Shonza, MUNGU akubariki sana. Huo ni mwanzo tu, tunategemea kukuona ukipaa.
Post a Comment