Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya
Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) MNEC
Salim Asas akiwahutubia wajumbe wa baraza kuu la umoja wa wanawake manispaa ya Iringa na kusema kuwa bado anaumizwa na matokeo ya ubunge wa jimbo la Iringa mjini baada
ya wapinzani kushinda kwa kishindo mwaka 2015 kwa ni kitendo ambacho
hakukitegemea.
Mwenyekiti wa umoja wa wanawake UWT manispaa ya Iringa Ashura jongo akimtoa hofu MNEC Salim Asas juu ya kukomba jimbo baada ya kulipoteza kwa kusalitia mwaka 2015
Baadhi ya wageni waliokuwa wamealikwa kwenye baraza hilo kwa ajili ya kujifunza na kutoa mapendekezo pale wanapopata nafasi
Baadhi ya viongozi wa chama cha mapinduzi mkoani Iringa walipokuwa wakimsikiliza kwa umakini mjumbe wa Halmashauri Kuu ya
Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) MNEC
Salim Asas alipokuwa anatoa ya moyo kuhusu kushindwa katika uchaguzi wa mwaka 2015
Na Fredy Mgunda,Iringa.
MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya
Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) MNEC
Salim Asas bado anaumizwa na matokeo ya ubunge wa jimbo la Iringa mjini baada
ya wapinzani kushinda kwa kishindo mwaka 2015 kwa ni kitendo ambacho
hakukitegemea.
Akizungumza wakati wa baraza la
UWT manispaa ya Iringa Asas alisema kuwa
usaliti ulifanywa katika uchaguzi wa mwaka 2015 umekuwa ukimuumiza hadi sasa na
kitendo anafikiri kitadumu moyoni mwake hata kwa miaka kumi kwakuwa bado
anakumbuka mara kwa mara.
“Naombeni niongee ukweli
kitendo kilichofanywa na wanaccm wa manispaa ya Iringa katika uchaguzi wa mwaka
2015 kilikuwa kitendo ambacho ni usaliti mkubwa ambao unaumiza sana kichwa changu”
alisema Asas
Asas alisema kuwa uchaguzi huo
kulikuwa na wanaccm wengi ambao mchana walikuwa ccm na usikuwa walikuwa kwa
wapinzani hivyo lazima tuondoe usaliti kwenye chama bila hivyo tutaendelea
kushindwa kila siku.
“Unakuta rasilimali zilizokuwa
zinatolewa na chama cha mapinduzi zote
zinatumika kwa wapinzani kuhakikisha wanaiangusha ccm,sasa hicho kitu ndio
ambacho kinaniumiza sana kichwa hadi hii leo” alisema Asas
Asas aliutaka umoja wa wanawake
(UWT) manispaa ya Iringa kufanya kazi kwa umoja unatakiwa na kuhakikisha kuwa
ccm inakuwa ila na isiyo na makundi ili kufika mwaka wa uchaguzi wanashinda kwa
kishindo kwa kutumia umoja wao.
“Nawaombe muutunze umoja huu
ambao sasa mnao hadi kipindi cha uchaguzi wowote ule ambao upo mbele yetu na
kuhakikisha kuwa tunashinda kila chaguzi kwa kishindo kwa kuwa nyie akina mama
ndio huwa mnakula ambazo haziamishiki” alisema Asas
Kwa upande wake mwenyekiti wa
UWT manispaa ya Iringa Ashura jongo alimuhakikishia MNEC Salim Asas kuwa kosa
lilofanyika mwaka 2015 halitajirudia tena katika chaguzi yoyote ambayo itakuwa
inafanyika katika manispaa ya Iringa.
“Ndugu MNEC kwa kweli
tumejifunza na tunajutia kitu kilichofanyika mwaka 2015 hivyo tunakuhadi kuwa
kwenye umoja wetu wa wanawake Manispaa ya Iringa hakitaa tokea kama
kilivyotokea,na tutashinda chaguzi zetu kwa kuwa kila mtu anaumia na
kilichotokea mwaka 2015” alisema Jongoo
Jongoo alimshukuru MNEC kwa
kurudisha umoja kwa wanaccm mkoa wa Iringa kwa kuwa anafanya kazi kubwa
kuhakikisha kila kitu kinakuwa kama kinavyokusudiwa na kuhakikisha umoja ambao
umetengenezwa na viongozi wapya unadumu hadi watakapomaliza uchaguzi.
“Mheshimiwa MNEC umoja ambao
tunao hivi sasa tunatakiwa kuulinda na kuudumisha hadi kipindi cha chaguzi zote
na kuhakikisha kuwa ccm inashinda kwa kushinda na kuendelea kuwa ngoja ya chama
hicho kama ilivyokuwa hapo awali” alisema Jongoo
No comments:
Post a Comment