ANGALIA LIVE NEWS

Friday, March 16, 2018

Shilole na Uchebe Wazungumzia Tetesi za Kuachana

Msanii wa muziki bongo ambaye kwa sasa amejikita zaidi katika ujasiriamali, Zuwena Mohamed maarufu kama Shilole au Shishi Trump, hatimaye amefunguka kuhusu kuvunjika kwa ndoa yake na mume wake Ustadhi Uchebe kufuatia posti ya ua jeusi iliyowekwa kwenye ukurasa wa Instagram ya Uchebe.
Uchebe amefunguka na kusema ni kweli akaunti ni yake na ua jeusi lilipostiwa na kusindikizwa na maneno yaliyoleta utata na kutafsiriwa na mashabiki kuwa ndoa hiyo imevunjika kama ambavyo uhusiano wa Diamond na Zari ulivyovunjika.

Uchebe amefafanua kuwa watu wasiojulikana waliiba akaunti yake na kufanya hayo ambayo yamefanyika na kutafsiriwa hivyo na mashabiki.

Aidha yeye na mke wake shilole wamewatoa hofu wananchi na mashabiki wao kua hawawezi kuachana na hawafikirii kuachana milele na pia ameongezea yupo sawa na mke wake hawajagombana kama ambavyo watu wanafikiria.


“Sio kweli sijaachana na mke wangu na wala hatufikirii kuachana, kuna watu wanafiki wanapenda kusikia tumeachana, kuhusu ile post kuna mtu alifanikiwa kuhack acount yangu na kupost vile lakini sijamuacha mke wangu, na wala hatuna ugomvi, na niwaambie tu kuwa hatuachani leo hata kiama”, amesema Uchebe.

Shilole na Uchebe walifunga ndoa mwishoni mwa mwaka jana, Ndoa yao ni moja kati ya ndoa ambazo zilifanya vizuri na kuvuma sana mitandaoni, huku ikiwa imehudhuriwa na wasanii mbalimbali ambao walitoa ahadi kedkede kwa maharusi hao.

Kufuatia tukio hilo linalosemekana wameachana wawili hao wamewatoa wasiwasi mashabiki na kusema kuwa sio kiki ila ni tukio amablo limefanywa na watu wasiojulikana ila wapenzi hao wapo pamoja na hawategemei kuachana siku za usoni.

No comments: