ANGALIA LIVE NEWS

Friday, April 20, 2018

UNESCO YAWANOA MAFUNDI MITAMBO WA REDIO ZA JAMII 25

Afisa Miradi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Rose Ngunangwa akifafanua jambo wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo mafundi mitambo wa radio za jamii 25 yaliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) yaliyoanza Aprili 19 hadi Aprili 25 mwaka huu.
Meneja wa Huduma za Ufundi kutoka TBC, Mhandisi Yusuph Afidhu akizungumza na washiriki kwenye mafunzo ya kuwajengea uwezo mafundi mitambo wa radio za jamii zilizopo Tanzania Bara na Zanzibar.
Mkuu wa Studio Redio ya TBC, Mhandisi Omary Salum akitoa mada kuhusu namna ya studio inavyobidi kuwa ili kuweza kurusha matangazo kistadi wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo mafundi mitambo wa radio za jamii 25 yaliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO).
Baadhi ya mafundi mitambo wa radio za jamii wakifuatilia mada kwenye mafunzo ya kuwajengea uwezo kwa mafundi mitambo wa radio za jamii 25 yaliyofanyika katika ukumbi wa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya mafundi mitambo wa radio za jamii wakichangia mada kwenye mafunzo ya kuwajengea uwezo kwa mafundi mitambo wa radio za jamii 25 yaliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) yaliyoanza Aprili 19 hadi Aprili 25 mwaka huu.
Baadhi ya mafundi mitambo wa radio za jamii wakiwa kwenye mafunzo ya vitendo kwenye kituo cha TBC cha Tazara wakati mafunzo ya kuwajengea uwezo kwa mafundi mitambo wa radio za jamii 25.

SHIRIKA la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), limeanza kutoa mafunzo ya siku saba kwa mafundi mitambo wa radio za jamii 25 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar.

Lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo katika utendaji kazi wao.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Shirika hilo jijini Dar es salaam, mafunzo hayo yanagusa masuala yanayozunguka jamii namna ya kuyafanya kifanisi na kitaalamu ili kuweza kurusha matangazo yaliyomazuri kwa jamii ambayo yameanza Aprili 19 hadi Aprili 25 mwaka huu.

"Washiriki hawa wanatoka katika radio 25 za jamii zinazosaidiwa na shirika letu.Kubwa ni kuwapa mafundi mitambo hao elimu kuhusu namna ya kuifanya radio ya jamii kuwa bora wakati wa urushwaji wa matangazo kwa jamii husika,"imesema.

Imeongeza Unesco kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Uswis (SDC) husaidia radio za jamii na mtandao wa radio za jamii (TADIO).

Ufadhili huo umelenga kuhakikisha wananchi wa Tanzania hasa wale wa vijijini wanafanya uamuzi sahihi kuhusu maisha yao kwa kupata taarifa sahihi kutoka redioni.

Washiriki wanaofadhiliwa na SDC ni Nuru FM (Iringa), Pambazuko FM (Morogoro), Fadhila FM (Mtwara) Jamii Mtukwao FM (Mtwara), Loliondo FM (Arusha), Baloha FM (Shinyanga), Kahama FM (Shinyanga) Ileje FM (Songwe),Tripple A FM (Arusha) na Storm FM (Geita).

Pia Sengerema FM (Mwanza), Kwizera FM (Kagera), Dodoma FM (Dodoma), Kitulo FM (Njombe), Uvinza (Kigoma), Mpanda (Katavi), Pangani (Tanga), Boma (Kilimanjaro), Mazingira (Mara), Mtegani FM (Kusini Unguja),mkoani FM (Kusini Pemba), Micheweni FM (Kaskazini Pemba),Tumbatu FM (Kaskazini Unguja) na Ruangwa FM (Lindi).

No comments: