Mgeni Rasmi, Mheshimiwa Dkt. Faustine Ndugulile, Naibu Waziri Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto akitoa hotuba wakati wa uzinduzi wa Uni Life Campus Program kwenye Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili, MUHAS.
Wafanyakazi na wanafunzi wa MUHAS wakifuatilia hotuba za uzinduzi wa Uni Life Campus Program kwenye Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili, MUHAS
Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo, Prof. Appolinary Kamuhabwa akizungumza katika sherehe za uzinduzi wa Uni Life Campus Program kwenye Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili, MUHAS.
Mbunge anaewakilisha Vyuo Vikuu katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwanzilishi wa Uni Life Campus Program, Mheshimiwa Esther Mmasi akielezea maono ya program hii wakati wa uzinduzi wa Uni Life Campus Program kwenye Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili, MUHAS
Dkt. Faustine Ndugulile, Naibu Waziri Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto akitoa ufafanuzi wa maswali yaliyoulizwa na wanafunzi wakati uzinduzi wa Uni Life Campus Program kwenye Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili, MUHAS.
Mgeni Rasmi, Mheshimiwa Dkt. Faustine Ndugulile, Naibu Waziri Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (ameketi katikati), Mbunge anaewakilisha Vyuo Vikuu katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwanzilishi wa Uni Life Campus Program, Mheshimiwa Esther Mmasi (wa pili kushoto), Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo, Prof. Appolinary Kamuhabwa (wa pili kulia), msemaji wa jeshi la polisi (kulia) na mwakilishi wa kutoka bodi ya mikopo (kushoto), wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa serikali ya wanafunzi wa MUHAS
Naibu Waziri Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuzindua Uni Life Campus Program kwenye Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili, MUHAS
Na Mwandishi Wetu.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile amezindua programu ya Uni Life Campus kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi, MUHAS.
Akizungumza katika uzinduzi wa programu hiyo, Dkt. Ndugulile amewahimiza wanafunzi wa MUHAS kuzingatia masomo pamoja na kupenda kujihusisha na mambo mengine kwenye jamii. Amesisitiza kuwa kama wanafunzi wa fani za afya wanao uwezo wa kujihusisha na programu mbalimbali zinazofikia jamii zenye uhitaji na kushiriki katika kutoa huduma za afya.
Akitoa mifano ya maisha yake kama mwanafunzi wa miaka ya nyuma wa Chuo hiki, Dkt. Ndugulile amesema katika maisha ni muhimu sana kuwa na malengo pamoja na mipango ya kuweza kufikia malengo hayo. Amesema nafasi mbalimbali zipo ila zinahitaji kujibidiisha hasa kwenye vikundi mbalimbali vya kitaaluma ili uweze kuzitambua nafasi hizo na kuziomba.
Naibu Waziri pia amewaasa wanafunzi kuwa makina na jinsi wanavyotumia mitandao ya jamii maana ina uwezo mkubwa wa kuwajenga kama wakitumia vizuri na kuwabomoa endapo ikitumika vibaya. "Watu wa afya ni kioo cha jamii hivyo basi ni muhimu kuzingatia maadili ya sekta hii na kuhakikisha tabia zenu zinaendana na mienendo yenu", aliongeza.
Akielezea maono ya programu hii, Mwanzilishi wa Uni Life Campus Program ambaye pia ni Mbunge anaewakilisha Vyuo Vikuu katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bi Esther Mmasi amesema mojawapo ya malengo la programu hii ni kuongeza kiwango cha kujitambua kwa wanafunzi ili kupunguza changamoto wanazokabiliana nazo wakiwa vyuoni.
Amesema programu hii pia imelenga kuongeza uelewa wa wanafunzi wa vyuo wa namna nzuri wa kutumia technolojia ya mawasiliano na pia kusisitizia matumizi mazuri ya mitandao ya kijamii.
Naye Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo, Prof. Appolinary Kamuhabwa amesema Chuo kinatambua umuhimu wa wanafunzi kupata maarifa yatakayo wawezesha kujitambua na kutambua nafasi walizo nazo ili waweze kuzitumia kikamilifu.
Kutokana na hilo, Prof. Kamuhabwa alisema Chuo kinatoa kipaumbele cha kutosha katika kuhakikisha wanafunzi hasa wa jinsia ya kike ambao mara nyingi ndio wahanga wakubwa wa changamoto mbalimbali za kimfumo, wanapatiwa semina za kuwajengea ujasiri na kuwa na mtazamo chanya katika maisha.
"Lengo kuu la kuwa na semina mbalimbali ni katika kuhakikisha wanafunzi wanafanya vizuri katika masomo yao bila kuwa na vizuizi vya masuala mengine ya kijamii ambayo yanaweza kuwakwamisha" aliongeza.
No comments:
Post a Comment