Advertisements

Tuesday, August 21, 2018

MWINYI, MKAPA, KIKWETE WAWASILI MWANZA KUELEKEA CHATO

Marais Wastaafu wa Tanzania, Ally Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete wamewasili jijini Mwanza leo Agosti 21, 2018 wakielekea Chato mkaoni Geita kuhudhuria mazishi ya Dada wa Rais Dkt. John Magufuli, Monica Magufuli anayetarajiwa kuzikwa baadaye leo.
Bi. Monica alifariki dunia Jumamosi iliyopita, Hospitali ya Bugando alikokuwa amelazwa akipatiwa matuibabu.
Wastaafu hao wamewasili na Ndege ya Air Tanzania katika Uwanja wa Ndege wa Mwanza uliyopo Ilemela na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela kabla ya kuelekea Chato mkoani Geita kujumuika na familia ya Magufli katika mazishi ya ndugu yao
Mzee Mkapa ameambatana na mkewe Mama Anna Mkapa na mzee Kikwete naye aliambatana na mkewe, Mama Salma Kikwete.

No comments: