Meneja Masoko wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) Anitha Rwehumbiza akikabidhi moja ya fulana kwa Mjumbe wa kamati ya utendaji ya Dodoma Footbal club (DFC) Yusuph Shaban Yusuph .SBL leo imetoa jozi 20 za jezi kwa timu ya Dodoma Foot-ball Club,makabidhiano hayo yamefanyika katika ofisi za SBl Temeke Jijini Dar es salaam.
Dar es Salaam, Agosti 29 2018 –Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) leo imetoa jozi 20 za jezi kwa timu ya Dodoma Foot-ball Club, hatua ambayo imepongezwa na timu hiyo inayojifua kuwania nafasi ya kucheza ligi kuu msimu ujao.
Msaada huo kwa mujibu wa Meneja Masoko wa SBL Anitha Rwehumbiza, ni muendelezo wa nia ya kampuni hiyo kuendeleza michezo pamoja na shughuli nyingine zinazowaleta watu pamoja.
“Kama ilivyo kwa mpira wa miguu ambao huwaunganisha na kuwaleta watu pamoja, SBL kupitia bia yake ya Serengeti Premium Lager inalenga kuwaunganisha Watanzania na kusaidia kujenga jamii imara na yenye umoja. Tunaamini michezo na hususani mpira wa miguu siyo tu inaunganisha watu bali pia inasaidia kuibua vipaji vya vijana wengi kwa manufaa ya jamii nzima,” alisema Anitha
Kwa upande wake Mjumbe wa kamati ya utendaji ya Dodoma Footbal club (DFC) Yusuph Shaban Yusuph aliishukuru kampuni ya SBL kwa msaada huo na kusema kuwa utasaidia kupunguza upungufu wa vifaa vya michezo unaoikabili timu hiyo.
SBL inahistoria kongwe ya kuthamini mpira wa miguu hapa nchini. Mwezi Mei 2017, iliingia mkataba wamiaka mitatu wa udhamini wa timu ya taifa, Taifa Stars wenye thamani ya shilingi bilioni 2.1
Udhamini wa timu ya taifa ulifuatiwa na mkataba mwingine wa miaka mitatu wa udhamini wa ligi ya mpira wa miguu kwa wanawake wenye thamani ya shilingi milioni 450. Mikataba yote miwili ya udhamini ilifanyika chini ya bia pendwa za SBL, Serengeti Premium Lager na Serengeti Premium Lite
MWISHO
No comments:
Post a Comment