MHESHIMIWA Jaji Dkt.
Eliezer M.Feleshi, Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, (aliyesimama)
akitoa hotuba ya ufunguzi wa mafunzo kwa mahakimu wakazi wa wilaya na mikoa ya
Dar es Salaam, Pwani, Lindi, Mtwara na Morogoro kuhusu Sheria ya Fidia kwa
Wafanyakazi Sura 263 marejeo ya mwaka
2015 iliyoanza Septemba 5, 2018 mkoani Morogoro. Semina hiyo imeratibiwa kwa
ushirikiano wa Chuo Cha Uongozi wa Mahakama Lushoto na Mfuko wa Fidia kwa
Wafanyakazi (WCF). Wengine pichani ni Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, ambaye
pia ni Mkuu wa Chuo hicho Dkt. Paul F. Kihwelo (kulia) na Mkurugezni Mkuu wa
WCF, Bw.Masha Mshomba.
Na
K-VIS BLOG/Khalfan Said, Morogoro
MHESHIMIWA
Jaji Dkt. Eliezer M.Feleshi, Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, amesema
hategemei kesi zinazohusiana na masuala ya fidia kwa wafanyakazi zikichelewa
pindi mashauri yake yanapofika mahakamani.
Dkt.
Feleshi ameyasema hayo Mjini Morogoro Septemba 5, 2018 wakati akifungua mafunzo
kwa mahakimu kutoka mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Mtwara, Lindi na Morogoro yanayoratibiwa
na Chuo Cha Uongozi wa Mahakama Lushoto na kuendeshwa na Mfuko wa Fidia kwa
Wafanyakazi (WCF) yanayofanyika kwa siku mbili kuanzia leo.
“Sitegemei
kesi za namna hii ziingie kwenye kundi la njoo kesho… njoo kesho, mashahidi
wake ni wangapi? Kesi za namna hii zikiingia
zisikilizwe mfululizo, kumbukeni inamuhusu mtu aliyeumia, inagusu uhai, inahusu
ulemavu wa kudumu kwa hiyo nyuma kuna wategemezi na yeye mwenyewe kwa hiyo
inahusu maisha ya mtu, pia ushahidi wake uko wazi na adhabu zake ziko bayana”
Alifafanua Dkt. Feleshi.
Aidha
Mhe. Jaji Kiongozi alisema, kila mfanyakazi aliyeumia au kuugua kutokana na
kazi anayo haki ya kupata fidia stahiki na kwa wakati kwa mujibu wa sheria na
kwa yule atakayefariki katika mazingira hayo basi wategemezi wake nao
wanapatiwa haki zao zilizoanishwa kisheria.
Alisema
huduma ya Hifadhi ya Jamii ni haki inayotambulika na kulindwa na Katiba, ibara
ya 11 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 pamoja na
mambo mengine inatamka kwenye ibara ndogo kwamba Mamlaka ya Nchi itaweka
utaratibu unaofaa kwa ajili ya kufanikisha utekelezaji wa haki ya mtu kufanya
kazi, haki ya kujipatia elimu na haki ya kupata msaada kutoka kwa jamii wakati
wa uzee, maradhi, au hali ya ulemavu na katika hali nyinginezo za mtu kuwa
hajiwezi, na bila kuathiri haki hizo Mamlaka ya Nchi itaweka utaratibu wa
kuhakikisha kwamba kila mtu anaishi kwa jasho lake.
“Hayo
ni maneno ambayo yamewekwa kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
kwa hiyo ni haki ambayo imetamkwa na inalidwa na Sheria na kwa kuzingatia
matakwa hayo ya kikatiba ndio maana ilitungwa sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi
iliyoanzisha Mfuko huu wa WCF.” Alifafanua Dkt. Feleshi.
Alisema
Mafunzo hayo kwa Mahakimu kuhusu utekelezaji wa sheria hiyo, yana manufaa
makubwa na ndio maana yameratibiwa na Chuo cha Uongozi wa Mahakama ambacho ndio chenye jukumu la kutoa
elimu kwa watumishi wa mahakama.
“Katika
sheria ya sasa kwa mujibu wa vifungu vya 22 (1) 46 na 48 na majedwali ya 2,3 na
4 ulipaji wa fidia unazingatia zaidi uhalisia wa tukio, kiwango cha hasara na
madhara ambavyo vinafanya fidia inayolipwa ikokotolewe kwa kufuata asilimia ya
vigezo hivyo na malipo ya ujira wa mwezi au malipo ya mwisho ya mhusika.”
Alibainisha Dkt. Feleshi.
“Takwimu
zinaonyesha kuwa Mfuko umekwishalipa Fidia kiasi cha Shilingi bilioni 4.4 tangu
ulipoanza kulipa fidia hadi Julai 31, 2018, na hii inaonyesha umuhimu wa Mfuko
huu kwa jamii, taifa lakini hata sisi wenyewe kama watumishi.” Alisema.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, Bw. Masha
Mshomba alisema kwa sasa Mfuko umeweka kipaumbele kwenye utoaji elimu kwa wadau
mbalimbali wakiwemo Waheshimiwa Mahakimu ili na wao waelewe vizuri shughuli za
Mfuko na jinsi ya kutekeleza sheria iliyoanzisha Mfuko.
Kwa
sasa Mfuko umekwisha wafikia wadau wengi na kumekuwepo na mabadiliko makubwa
katika uelewa wa kutekeleza sheria hii na ni wachache sana ambao bado wanakuwa
wazito kutekelza sheria, alisema Bw. Mshomba.
Washiriki
wa mafunzo hayo wanatarajiwa kujifunza sheria inayosimamia shughuli za Mfuko,
lakini pia muundo na shighuli za Mfuko na taratibu za utoaji Fidia.
Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba, akizungumza kwenye semina hiyo.
Baadhi ya Wahwshimiwa Mahakimu Wakazi Wafawidhi wa Mahakama nchini.
Mheshimiwa Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Kisarawe Mkoani Pwani, Mhe. Devota Kisoka.
Mhe. Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mtwara, Bi.Elizabeth S. Missana, akipitia kipperushi chenye maelezo kuhusu shughuli za Mfuko.
Baadhi ya Waheshimiwa Mahakimu Wakazi Wafawidhi wa Mahakama nchini.
Hakimu Mfawidhi wa Mahaka ya Hakimu Mkazi Morogoro, Mheshimiwa Elizabeth Nyembele, akizungumza kwenye semina hiyo.
Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Kibaha, Mhe.Joyce J. Mkhoi, akitoa maoni yake kwenye semina hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba, akishauriana jambo na Mkuu wa Huudma za Sheria wa Mfuko huo, Bw.Abraham Siyovelwa
Bw. Mshomba (katikati), akimtambulisha Dkt. Feleshi kwa Mkurugenzi wa Uendeshaji WCF, Bw. Anselim Peter, wakati akiwasili ukumbini.
Dkt. Feleshi akisalimiana na Bw. Siyovelwa.
MHESHIMIWA Jaji Dkt.
Eliezer M.Feleshi, Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, (kushoto), na
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Bw. Masha Mshomba,
wakiwa na furaha baada ya Dkt. Felishi kufungua mafunzo ya kujenga uwezo na
uelewa wa sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi Kifungu namba 5 [Sura ya 263
iliyofanyiwa marejeo mwaka 2015] kwa mahakimu Wakuu Wakazi wa Mikoa na Wilaya
kutoka mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Morogoro, Lindi na Mtwara. Semina hiyo
iiyoandaliwa kwa ushirikiano kati ya Chuo Cha Uongozxi wa Mahakama Lushoto na
Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) imeanza Septemba 5, 2015 mjini Morogoro.
Kutoka kushoto ni Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Mhe. Godfrey Isaya, Mhe. Dkt. Feleshi, Mhe. Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania na Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto, Mhe. Dkt. Jaji Paul Kihwelo, Mkuu wa Huduma za Sheria WCF, Bw. Abraham Siyovelwa.
Mkuu wa Huduma za Sheria WCF, Bw. Abraham Siyovelwa, akitoa mada kuhusu sharia zinazosimamia Mfuko huo.
Mkurugenzi wa Uendeshaji WCF, Bw. Anselim Peter, akitoa mada |
Afisa Uhusiano na Mawasiliano Mwandamizi wa WCF, Bw. Sebera Fulgence, akiongoza semina hiyo. |
MHESHIMIWA
Jaji Dkt. Eliezer M.Feleshi, Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, akisalimiana na Afisa Sheria wa WCF, Bw. Deo Victor.
Mhadhiri Msaidizi wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA), Mhe.Lamek Samson akiwa na Afisa Uhusiano na Mawasiliano Mwandamizi wa WCF, Bw. Sebera Fulgence.
No comments:
Post a Comment