Mwenyekiti wa Bunge na Mbunge wa Ilala, Mhe. Mussa Zungu (kushoto)
akizungumza na Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Mhe. Dan Kazungu (kulia)
alipomtembelea leo Bungeni Mjini Dodoma. Katika mazungumzo hayo Mhe.
Zungu alimuwakilisha Spika wa Bunge. Balozi huyo ambae ni mpya alikuja
kwa lengo la kujitambulisha kwa Mhe. Spika na kumueleza nia ya kujenga
jengo lao la Ubalozi wa Kenya hapa Jijini Dodoma katika vile viwanja
walivyopewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe
Magufuli.
Mwenyekiti wa Bunge na Mbunge wa Ilala, Mhe. Mussa Zungu (kushoto)
akimsikiliza Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Mhe. Dan Kazungu (kulia)
alipomtembelea leo Bungeni Mjini Dodoma. Katika mazungumzo hayo Mhe.
Zungu alimuwakilisha Spika wa Bunge. Balozi huyo ambae ni mpya alikuja
kwa lengo la kujitambulisha kwa Mhe. Spika na kumueleza nia ya kujenga
jengo lao la Ubalozi wa Kenya hapa Jijini Dodoma katika vile viwanja
walivyopewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe
Magufuli.
Mwenyekiti wa Bunge na Mbunge wa Ilala, Mhe. Mussa Zungu (kushoto)
akisalimiana na Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Mhe. Dan Kazungu
(kulia) alipomtembelea leo Bungeni Mjini Dodoma, kwa Katika mazungumzo
hayo Mhe. Zungu alimuwakilisha Spika wa Bunge, Pia Balozi huyo ambae ni
mpya alikuja kwa lengo la kujitambulisha kwa Mhe. Spika na kumueleza nia
ya kujenga jengo lao la Ubalozi wa Kenya hapa Jijini Dodoma katika vile
viwanja walivyopewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
John Pombe Magufuli.
Mbunge wa Muleba Kusini, Mhe. Anna Tibaijuka (kushoto) akiteta jambo na
Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Mhe. Dan Kazungu alipomtembelea leo
Bungeni Mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa Bunge na Mbunge wa Ilala, Mhe. Mussa Zungu anaemuwakilisha
Spika Ndugai, Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi
wakimsikiliza Ofisa Mtendaji Mkuu wa Baraza la Taifa la Watu Wanaoishi
na Virusi vya Ukimwi Tanzania (NACOPHA), Ndg. Deogratius Rutatwa (Kulia)
wakati akiwashukuru Waheshimiwa kwa Kujitoa katika Shughuli Mbali mbali
zinazohusiana na Baraza hilo, moja wapo likiwa ni upimaji wa Virusi
vya Ukimwi kwa hiari.
Mwenyekiti wa Bunge na Mbunge wa Ilala Mhe. Mussa Zungu (katikati)
anaemuwakilisha Spika Ndugai akikabidhiwa cheti kutoka kwa Ofisa
Mtendaji Mkuu wa Baraza la Taifa la Watu Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi
Tanzania (NACOPHA), Ndg. Deogratius Rutatwa (Kushoto) ikiwa ni Shukrani
kwa Kujitoa kwao katika Shughuli Mbali mbali zilizoratibiwa na Baraza
hilo, moja ya tukio likiwa ni upimaji wa Virusi vya Ukimwi kwa hiari,
baada ya kikao kilichofanyika leo Bungeni Jijini Dodoma. kulia ni
Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi, Mhe. Oscar
Mukasa
Mwenyekiti wa Bunge na Mbunge wa Ilala, Mhe. Mussa Zungu (mwenye tai
nyeusi mbele), anaemuwakilisha Spika Ndugai akiwa katika picha ya pamoja
na Wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi na
Watendaji Wakuu kutoka Baraza la Taifa la Watu Wanaoishi na Virusi vya
Ukimwi Tanzania (NACOPHA), baada ya kikao kilichofanyika Bungeni Jijini
Dodoma. Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya
Masuala ya Ukimwi, Mhe. Oscar Mukasa na kulia kwake ni Ofisa Mtendaji
Mkuu wa Baraza la Taifa la Watu Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi Tanzania
(NACOPHA), Ndg. Deogratius Rutatwa (Kulia)
Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi, Mhe.
Oscar Mukasa (katikati) akizungumza na ugeni kutoka Ubalozi wa Marekani
wanahusika na utekelezaji wa Miradi ya Ukimwi, Wajumbe wa kamati hiyo.
Ugeni ulioongozwa na Mratibu Mkazi wa PEPFAR, Ndg. Brian Rettmann (kulia
kwake) katika kikao kilichofanyika leo Bungenii Jijini Dodoma.
(PICHA NA DEONISIUS SIMBA - OFISI YA BUNGE)
No comments:
Post a Comment