Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais , Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora Mhe. Geogre Mkuchika akieleza umuhimu wa muswaada wa Sheria
ya Bodi ya Taaluma ya Walimu Tanzania, 2018. (The Tanzania Teachers
Professional Board Act, 2018) wakati wa kupitishwa kwa muswaada huo leo
Bungeni Jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe.
Mussa Sima akieleza mikakati ya Serikali kuhakikisha inatunza mazingira
ya ziwa manyara ili kuondoa athari za mabadiliko ya tabia nchi.
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Joyce Ndalichako
akisisitiza jambo wakati akijibu hoja za wabunge leo Bungeni Jijini
Dodoma wakati wa kupitisha muswaada wa Sheria ya Bodi ya Taaluma ya
Walimu Tanzania, 2018. (The Tanzania Teachers Professional Board Act,
2018).
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Jumaa Aweso akisisitiza
mikakati ya Serikali kuhakikisha kuwa wananchi wote wanafikiwa na huduma
ya maji safi na salama kote nchini.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji akisisitiza kuhusu
hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kuhakikisha kuwa wananchi
waliokuwa na akaunti katika iliyokuwa Benki ya FBME wanalipwa haki zao
kwa mujibu wa sheria na Kanuni za utumishi baada ya Benki hiyo
kufungwa.
Naibu
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angelina Mabula
akieleza hatua zilizochukuliwa na Serikali kuondoa mgogoro kati ya
wananchi na Manispaa ya Mtwara Mikindani unaotokana na eneo la Mjimwema
na Tangira lililopimwa kwa ubia kati ya Manispaa na Taasisi ya UTT-PID
mwaka 2003.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa Mhe. Rita Kabati akisisitiza kuhusu
umuhimu wa wananchi kupata huduma bora za maji safi na salama wakati wa
kipindi cha maswali na majibu leo Bungeni Jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Bunge Mhe. Mussa Zungu akisisitiza jambo wakati wa
kupitishwa kwa muswaada wa Sheria ya Bodi ya Taaluma ya Walimu Tanzania,
2018.(The Tanzania Teachers Professional Board Act, 2018) leo Bungeni
Jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge Kazi, Vijana, Ajira
na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama akisisitiza jambo kwa Naibu
Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe. Mussa
Sima, leo Bungeni Jijini Dodoma.
Sehemu ya wageni waliofika Bungeni kama wanavyoonekana katika picha. (Picha zote na Frank Mvungi)
No comments:
Post a Comment