Mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi akiwa ameongozana na mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela pamoja na meneja wa uwanja wa nduli Anna Kibopile alipofanya ziara katika uwanja wa ndege wa Nduli kwa kufahamu maendeleo ya ukarabati mdogo wa uwanja huo na kubaini baadahi ya changamoto zinaukabili uwanja huo hasa katika swala la majengo kuto kidhi mahitaji ya wasafiri
Mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi akiwa ameongozana na mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela pamoja na meneja wa uwanja wa nduli Anna Kibopile wakiwa kwenye eneo ambalo linafanyiwa ukarabati mdogo
Mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi akiwa ameongozana na mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela wakipata maelezo kutoka kwa meneja wa uwanja wa nduli Anna Kibopile juu ya ukarabati wa uwanja unaoendelea
Mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi akiwa ameongozana na mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela pamoja na kamanda wa police mkoa wa Iringa Juma Bwire wakiangalia jengo la wasafiri katika uwanja wa nduli mkoani Iringa
Mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi akiwa ameongozana na mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela pamoja na meneja wa uwanja wa nduli Anna Kibopile wakiwa ndani katika sehemu ya abiri ambao wanasubiri kusafiri.
Mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi akiongea na waandishi wa habari wakati wa ziara katika uwanja wa nduli na kubaini mapungufu mengi ikiwapo gari hilo ambalo linaonekana la zimamoto ambalo toka lifike hapo halijawi kufanya kazi kutokana na kuwa bovu na spea zake kutopatikana.
NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
MKUU wa mkoa wa Iringa Ally
Hapi hajaridhishwa na hali halisi ya uwanja wa ndege wa nduli uliopo kata ya
nduli kuelekea kuijenga Iringa mpya kwa maendeleo ya wanairinga.
Akizungumza wakati wa ziara
ya kukagua ukarabati mdogo unaoendelea katika uwanja huo,hapi alisema kuwa
uwanja huo wa ndege unahitaji ukarabati wa maana ili kukidhi mahitaji ya
watumiaji na kukuza maendeleo ya wananchi wa mkoa wa Iringa.
“Nimetembea kwenye maeneo
mengi ya uwanja huu hayaridhi wala hayavutii kwa wawekezaji kuja mkoani hapa
kwa kuwa saizi wawekezaji wengi wanapenda kutumia usafiri wa anga hivyo ni
lazima kuwa na kiwanja cha ndege ambacho kitakidhi na kuvutia watalii na
wawekezaji wanapokuja mkoani hapa” alisema Hapi
Hapi alisema kuwa jengo la
wageni la uwanja huo ni dogo,halina ubora unaotakiwa na halikidhi kuwa katika uwanja
huo ambao hivi karibuni utaanza kupokea wageni wengi kutoka maeneo mbalimbali
ya ndani ya nje ya nchi.
“Sehemu hii ya kupumzikia
wageni hakuna,sehemu ya wasafiri wanapoongokea bado ni ndogo na haina vigezo
vya kuwa eneo la kupuzikia wasafiri,vyoo havifai eneo lenyewe bado halina
miundombinu ya kisasa ambayo itawavutia watu wengi kuja mkoani Iringa hivyo tunahitaji
kujenga jengo jipya na la kisasa kabisa” alisema Hapi
Haiwezekani uwanja wa ndegehuu
ukawa unamajengo na vifaa vingi ambavyo
vimechoka na havikizi mahitaji ya kuijenga Iringa mpya hivyo ni lazima kuwekeza
kwenye uwanja ili kuvutia wawekezaji na watalii ambao watakuja mkoani hapa.
Hapi aliongeza kuwa uwanja
wa ndege wa Nduli hauna hapa gari la fire ambalo litasaidia kuongoa majanga
yoyote yatakayotokea kwenye uwanja huu,hivyo ni lazima tserikali ijue kuwa
tunahitaji kuwa na gari la fire hapa kwa kuwa Iringa ni kitovu cha utali nyanda
za juu kusini.
“Nimejionea hapa mwenyewe
kuwa hakuna gari la fire linalofanya kazi kwa kuwa lililopo ni bovu na haliwezi
kutengenezeka kwa kuwa liltengenezwa kwenye viwanda vya miaka mingi iliyopita
na spea zake hazipatika hata nje ya nchi kwa mjibu wa wataalamu ambao
wamenieleza hapa” alisema Hapi
Hapi alisema kuwa gari ambalo
lipo katika uwanja wa ndege wa Nduli halijawahi kufanya kazi toka liletwe na
inasadikiaka kuwa litengenezwa miaka ya themanini huko hivyo hakuna gari la
zimamoto katika eneo hili hivyo ni
hatari kwa watumiaji wa uwanja huu.
Aidha hapa alisema kuwa
uwanja wa ndege wa Nduli unaumuhimu mkubwa wa kukuza uchumi wa mkoa wa Iringa
kwa kuwa watalii na wawekezaji wengi watautumia uwanja huu wa ndege kufanya
kazi kwa muda muafaka na kurudi walikotoka kwa kutumia usafiri wa anga.
“Ukiwa na uwanja wa ndege
ambao unakidhi vigezo vinavyotakiwa utasaidia kuongeza utalii wa kusini kama
ambavyo unajua kuwa Iringa ndio kitovu cha utalii na kuvutia wawekezaji wengi
ambao mara nyingi wamekuwa wakitumia usafiri wa anga tofautia wachache ambao
wamekuwa wakitumia usafiri wa barabara za chini” alisema Hapi
Naye meneja wa uwanja wa
ndege wa Nduli Anna Kibopile alisema kuwa jengo la abiria halikidhi mahitaji
kupokea abiri wengi ambao pia watakuwa wakitumia ndege ya serikali aina ya Bombardie
ambayo itaanza safari mkoani Iringa hapo baadae.
“Unajua kuwa ndege yetu ya Bombardie
ataanza safari ya kuja hapa mkoani hiyo itakuwa inachukua abiria wengi sana
hivyo jengo letu la abiria halitoshi kuwahudumia wasafiri ambao watakuwa
wakiutumia unjwa huo kufanya safari zao” alisema Kibopile
Kibopile alisema kuwa ndege ya Bombardie inabeba abira
zaidi ya sabini hivyo ni lazima kuhakikisha tunataua au tunajenga jengo kubwa
la abira ambalo mkuu wa mkoa wa iringa ameshauri kuwa jengo hilo halikidhi
mahitaji ya abiria ambao watakaokuwa wanakuja mkoani Iringa.
No comments:
Post a Comment