ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, November 14, 2018

MAANDALIZI YA MPANGO NA BAJETI KWA MWAKA 2019/20 KUZINGATIA MAONI YA WABUNGE

 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akijibu hoja mbalimbali za wabunge kabla ya kuhitimishwa kwa mjadala wa Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na Mwongozo wa Maadalizi ya Mpango na Bajeti ya Mwaka 2019/2020, Jijini Dodoma.
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), akijibu hoja mbalimbali za wabunge kabla ya kuhitimishwa kwa mjadala wa Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na Mwongozo wa Maadalizi ya Mpango na Bajeti ya Mwaka 2019/2020, Jijini Dodoma.
 Viongozi waandamizi wa Wizara ya Fedha na Mipango wakifuatilia mjadala wa wabunge, kabla ya kuhitimishwa kwa mjadala wa Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na Mwongozo wa Maadalizi ya Mpango na Bajeti ya Mwaka 2019/2020, Jijini Dodoma jana, Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Khamis Shaaban
 Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA- Bw. Charles Kichere (kushoto) na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu (wa pili kushoto) na Viongozi wengine waandamizi wa Wizara ya Fedha na Mipango wakifuatilia mjadala wa wabunge, kabla ya kuhitimishwa kwa mjadala wa Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na Mwongozo wa Maadalizi ya Mpango na Bajeti ya Mwaka 2019/2020, Jijini Dodoma jana.
 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (katikati), wakiwa katika picha ya pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Dkt. Adelardus Kilangi (Mb) (kulia), baada ya kuhitimishwa kwa mjadala wa Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na Mwongozo wa Maadalizi ya Mpango na Bajeti ya Mwaka 2019/2020, Jijini Dodoma jana.
 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) akipongezwa na Mbunge wa Viti Maalum (CHADEMA) Mhe. Dkt. Sware Semesi na Wabunge wengine akiwemo Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Dkt. Adelardus Kilangi (Mb) (kulia), nje ya ukumbi wa Bunge baada ya kuhitimishwa kwa mjadala wa Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na Mwongozo wa Maadalizi ya Mpango na Bajeti ya Mwaka 2019/2020, Jijini Dodoma jana.
 Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Dkt. Adelardus Kilangi (Mb) (kulia) akiteta jambo na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), nje ya Ukumbi wa Bunge, baada ya kuhitimishwa kwa mjadala wa Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na Mwongozo wa Maadalizi ya Mpango na Bajeti ya Mwaka 2019/2020, Jijini Dodoma jana.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Khamis Shaaban (kulia) akijadili jambo na Mbunge wa Witi Maalum Mhe. Mama Salma Kikwete (kushoto) na aliyewahi kuwa Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Saada Nkuya (Mb),  nje ya Ukumbi wa Bunge, baada ya kuhitimishwa kwa mjadala wa Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na Mwongozo wa Maadalizi ya Mpango na Bajeti ya Mwaka 2019/2020, Jijini Dodoma jana.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango)


Na Saidina Msangi na Farida Ramadhani-WFM
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) amesema kuwa Serikali itazingatia maoni na ushauri wa wabunge wote katika Maandalizi ya Mpango na Bajeti kwa Mwaka 2019/2020.

Waziri Mpango alitoa kauli hiyo Bungeni wakati akiahirisha mjadala wa Mapendekezo ya Serikali ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2019/2020.

Akitoa ufafanuzi wa baadhi ya  maoni ya wabunge kuhusu kuboresha sekta ya kilimo  ikiwemo kuongeza bajeti ya kilimo, Dkt. Mpango alisema kuwa uongezaji wa bajeti ya kilimo ni muhimu lakini lazima ufanyike kwa ulinganifu wa mahitaji ya kibajeti ya sekta nyingine muhimu.

“Ni muhimu kukumbuka kuwa sekta ya kilimo ina mwingiliano mkubwa na sekta nyingine. Mwenendo bora wa kilimo unategemea sana uwekezaji wa sekta saidizi hasa miundombinu ya umwagiliaji, barabara vijijini, umeme kwa ajili ya kuendesha viwanda vya kuongeza thamani ya mazao, uzalishaji wa zana za kilimo, dawa, elimu na afya kwa wakulima” alisema Waziri Mpango.

Aidha, waziri Mpango aliongeza kuwa ni muhimu kuvutia sekta binafsi kuwekeza katika sekta za kilimo na uvuvi, kuimarisha upatikanaji wa mikopo kwa wakulima, wafugaji na wavuvi pamoja na kutafuta masoko ya kikanda na kimataifa.

Akizungumzia miradi mikubwa inayotajwa kukwama Waziri Mpango alifafafanua kuwa miradi iliyokwama imetokana na masharti hasi ya wawekezaji ambayo hayana maslahi kwa Taifa.

“Serikali ina nia ya kuona nchi inaendelea haraka hata hivyo inayo dhamana ya kuhakikisha kuwa rasilimali hizo zinatumika vizuri kwa kulinda maslahi mapana ya Taifa” alisema Dkt. Mpango

Kuhusu kupungua kwa ukwasi katika uchumi waziri ameeleza kuwa madai hayo yanahusishwa na kupungua kwa fedha mifukoni kwa wananchi na kwa benki za biashara kwani upatikanaji wa fedha kwa mianya isiyo halali umedhibitiwa, ukwepaji kodi, madai hewa , ufisadi, rushwa, wizi, ubadhilifu wa mali ya umma vimekomeshwa.

Ametoa wito kwa wananchi kujishughulisha katika shughuli halali  na kufanya kazi kwa bidii na ufanisi ili kujenga Taifa na kufikia azma ya ujenzi wa uchumi wa viwanda.


Pia, Waziri Mpango ametoa rai kwa wabunge kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya tano katika kuwaletea wananchi maendeleo.  

No comments: