Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akiwaongoza Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Kilindi kuingia Kituo cha Polisi cha Songe, ikiwa ni ziara ya kikazi ya Naibu Waziri kukagua shughuli za ulinzi na usalama wilayani Kilindi mkoani Tanga .Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza katika kikao cha ndani kilichohusisha Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Kilindi ikiwa ni ziara ya kikazi ya Naibu Waziri kukagua shughuli za ulinzi na usalama wilayani Kilindi mkoani Tanga . Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kilindi, Sauda Mtondoo na Kulia ni Katibu Tawala wa Wilaya hiyo, Warda Abeid.
Mkuu wa Wilaya ya Kilindi, Sauda Mtondoo akizungumza katika kikao cha ndani kilichohusisha Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Kilindi ikiwa ni ziara ya kikazi ya Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati) kukagua shughuli za ulinzi na usalama wilayani Kilindi mkoani Tanga . Kulia ni Katibu Tawala wa Wilaya hiyo, Warda Abeid.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Kamishna Msaidizi Mwandamizi , Edward Bukombe, akizungumza katika kikao cha ndani kilichohusisha Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Kilindi ikiwa ni ziara ya kikazi ya Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani, ) kukagua shughuli za ulinzi na usalama wilayani Kilindi mkoani Tanga . Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Na Mwandishi Wetu
Serikali imedhamiria kujenga Vituo vya Polisi 65 katika wilaya mbalimbali nchini ikiwa ni juhudi za kukabiliana na uchakavu na upungufu wa vituo vya polisi nchini.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni baada ya kutembelea na kukagua Kituo cha Polisi cha Songe ambacho ndio kituo kikuu katika Wilaya ya Kilindi mkoani Tanga
Alisema Serikali inatambua changamoto za vituo vya polisi ikiwemo uchakavu, udogo wa majengo katika vituo mbalimbali nchini na iko katika mpango wa kujenga vituo vya polisi 65 ili kuwepo na ulinzi thabiti wa raia na mali zao.
“Serikali inatambua changamoto ya vituo vya polisi hasa katika wilaya mpya nchini, ikiwepo uchakavu wa majengo, kwahiyo uko mkakati maalumu wa kujenga vituo vya polisi 65 nchi nzima ili kuweza kukabiliana na matukio ya kiuhalifu, lengo la serikali ni kuhakikisha raia wake na mali zao zinakua salama na matukio ya kiuhalifu yanapungua na kutoweka kabisa,” alisema Masauni
Alisema Serikali pia inakaribisha nguvu za wananchi na wadau mbalimbali ambao wako tayari kusaidia ujenzi wa vituo vya polisi huku akipongeza baadhi ya maeneo nchini ambako vituo vya polisi vimejengwa kwa ushirikiano wa michango ya wananchi na serikali.
Awali akitoa taarifa ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Kilindi, Mkuu wa Wilaya ya Kilindi na Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama, Sauda Mtondoo alisema hali ya uhalifu kuanzia kipindi cha Januari hadi Oktoba 2018 ilikua ya wastani huku kukiripotiwa upungufu wa makosa kwa asilimia 9.8 kati ya mwaka 2018 na 2017.
“Kwa mujibu wa takwimu za uhalifu kulikuwa na jumla ya makosa makubwa ya jinai 163 ndani ya mwaka huu yaliyoripotiwa kwa kulinganisha na makosa 179 yaliyoripotiwa ndani ya mwaka 2017, ukiwepo upungufu wa makosa 16 katika vipindi hivyo viwili,” alisema Sauda
Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mbunge wa Kilindi, Omari Kibua alimshukuru Naibu Waziri kwa kufika jimboni hapo kujionea hali halisi ya kituo hicho kikuu cha wilaya baada ya kumuomba kufanya hivyo wakati wa kikao cha bunge kilichomalizika hivi karibuni.
No comments:
Post a Comment