Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akiwasili katika shule ya Sekondari Mikalanga akiongozana na Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Mhe. Cosmas Nshenye na Mbunge wa Viti Maalum kwa mkoa wa Ruvuma Mhe. Jacquiline Ngonyani kwenda kushirikiana na wananchi katika ujenzi wa bweni la wasichana shuleni hapo.
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akiangalia kikundi cha ngoma za asili katika shule ya Sekondari Mikalanga akiongozana na Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Mhe.Cosmas Nshenye na Mbunge wa Viti Maalum kwa mkoa wa Ruvuma Mhe. Jacquiline Ngonyani kwenda kushirikiana na wanachi katika ujenzi wa bweni la wasichana shuleni hapo.
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akishirikiana na Mbunge wa Viti Maalum kwa mkoa wa Ruvuma Mhe. Jacquiline Ngonyani katika ujenzi wa bweni la wasichana katika Shule ya Sekondari Mikalanga.
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akizungumza na wananchi waliojitokeza kushirki katika ujenzi wa bweni la wasichana katika shule ya Sekondari Mikalanga ikiwa ni juhudi za wananchi kupunguza adha ya watoto wa kike kupata mimba shuleni.
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akikabidhi mmoja ya mifuko 50 aliyochangia katika ujenzi wa bweni la wasichana katika shule ya sekondari Mikalanga ikiwa ni juhudi za wananchi kupunguza adha ya watoto wa kike kupata mimba shuleni.
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akicheza ngoma pamoja na wananchi wa Kata cha Muhagawa Wilayani Mbinga Mkoani Ruvuma wakati alipotembelea na kushiriki ujenzi wa Zahanati ya Kata hiyo wa pili kushoto ni Mbunge wa Viti Maalum kwa mkoa wa Ruvuma Mhe. Jacquiline Ngonyani
Baadhi ya Wananfunzi kutoka chuo cha Maendeleo ya Jamii Mlale wakishiriki kubeba matofali kuunga mkono juhudi za wananchi katika ujenzi wa moja ya Zahanati zilizopo katika Wilayaya Mbinga mkoani Ruvuma.
Jengo la bweni la wasicha katika Shule ya Sekondari Mikalanga lilkiwa katika hatua ya rental ikiwa ni juhudi za wananchi kuondokana na atha ya wasichana kutembea umbali mrefu kwenda shule mabapo wanakutana na changamoto nyingi ikiwemo mimba za utotoni zinazokatisha ndoto za watoto wa kike walio wengi nchini. Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW
Na Mwandishi Wetu Mbinga
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile ameitaka jamii kuwawezesha watoto wa kike kupata elimu ili kuwa na Jamii yenye mabinti wasomi na kuondokana na ukandamizaji wa watoto wa kike na wanawake.
Dkt. Ndugulile ametoa rai hiyo wilayani Mbinga mkoani Ruvuma wakati akishirikiana na wananchi katika ujenzi wa Bweni la shule ya Sekondari Mikalanga ambalo kwa kiasi kikubwa wananchi wametoa nguvu zao katika kufanikisha ujenzi huo.
Dkt. Ndugulile amesisitiza kuwa suala la elimu kwa mtoto wa kike na muhimu kutokana na changamoto za mtoto wa kike hasa suala la mimba za utotoni ambazo zinapelekea kupotea kwa ndoto za wanafunzi wa kike wengi.
Naibu Waziri Ndugulile amesema kuwa kwa mujibu wa takwimu zilizopo Mtoto mmoja kati ya watoto watatu wa kike hupata mimba za utotoni na kukatisha ndoto za Mtoto wa kike kupata elimu kati ya miaka 15 mpaka 19 ikiwa sawa na asilima 27.
"Tunataka taifa la mabinti waliosoma, madaktari, wahandishi na wataalam wengine tuunge mkono juhudi hizi ili tuondokane na na changamoto zinazopelekea watoto wa kike kupata mimba za utotoni" alisisitiza Dkt. Ndugulile.
Kwa upande wake Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Ruvuma Mhe. Jacquiline Ngonyani amemshukuru Naibu Waziri kwa kuamsha ari na kutoa mchango wake wa mifuko 50 ya Saruji ili kufanikisha watoto wa kike kupata elimu na kuondokana na changamoto za kukosa mabweni inayosababisha watoto wengi kupata mimba.
Akitoa taarifa ya Mradi kwa niaba ya wananchi mjumbe wa Kamati ya ujenzi wa Bweni hilo Inviolatha Lupogo amesema kuwa hadi kukamilika kwa mradi huo utagharimu kiasi cha Shillingi 139 ambapo mchango wa wananchi unatarajiwa kuwa ni Shillingi Millioni 43 na hadi sasa wananchi wamechangia shillingi Millioni 11
Ameongeza kuwa lengo la mradi huo ni kupunguza adha ya kutembea umbari mrefu , kuwapangisha watoto wa kike kiholela ambapo kwa mwaka 2017/2018 jumla ya watoto wa kike 12 walikatishwa masomo yao sababu ya ujauzito.
Mmoja wa wajumbe wa Kamati ya ujenzi wa Bw. Lilbrad Kinunda amesema kuwa wamefurahishwa na ujio wa Naibu Waziri Ndugulile na kushirikina na wananchi katika ujenzi wa bweni hilo na wao wanaunga mkono juhudi hizo kwa kujitolea katika kujenga bweni hilo kwa amasa zaidi.
Katika kuuunga mkono juhudi za wananchi wa Mikalanga Naibu Waziri Dkt. Ndugulile alitoa jumla ya mifuko 50 ya saruji na Mbunge wa Viti maalum mkoa wa Ruvuma Mhe. Jacquiline Ngonyani amechangia jumla ya mifuko 30 ya saruji.
No comments:
Post a Comment