Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikagua Kadi inayoonesha Idadi ya Dawa katika Chumba cha dawa, wakati akiwa katika ziara yake ya kukagua hali ya utoaji huduma za Afya katika Hospitali teule ya Rufaa ya Mkoa wa Mtwara Ligula.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikagua Idadi ya Wagonjwa waliosajiliwa kwenye mfumo, wakati akiwa katika ziara yake ya kukagua hali ya utoaji huduma za Afya katika Hospitali teule ya Rufaa ya Mkoa wa Mtwara Ligula.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akipokea daftari la mama aliyemleta mwanae kupata huduma katika Hospitali teule ya Rufaa ya Mkoa wa Mtwara Ligula, wakati akiwa katika ziara yake ya kukagua hali ya utoaji huduma za Afya katika Hospitali hiyo. Wakatikati ni Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo Dkt. Lobikieki Kissambu.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikagua mkoba wa Vifaa vya kujifungulia, wakati wa ziara yake ya kukagua hali ya utoaji huduma za Afya katika Hospitali teule ya Rufaa ya Mkoa wa Mtwara Ligula.
Na WAMJW - MTWARA
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile amewaasa watumishi wa wekta ya afya nchini kuacha tabia ya kufanya kazi kwa mazoea, na wajikite katika kutoa huduma kulingana na sheria na taratibu za taaluma zao.
Ameyasema hayo leo wakati alipofanya ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma za afya kwa wananchi katika Hospitali teule ya Rufaa ya Mkoa wa Mtwara - Ligula.
Katika ziara hiyo Dkt. Ndugulile amesema kuwa licha ya jitihada za kuboresha huduma za afya kwa wananchi, ni wajibu wa kila mtoa huduma za afya nchini kuhakikisha anatimiza wajibu wake bila shurti na kuacha kufanya kazi kwa mazoea.
"Nyinyi mnafanya kazi kwa mazoea, kwa nini hamjajaza taarifa wala kusaini katika fomu ya wagonjwa, na hili linaendana na maelekezo ambayo Serikali tunawapa, kwamba kila mtu aandike tarehe na muda ambao amefanya kazi, nyinyi maabara hamfanyi" alisema Dkt. Ndugulile
Pia, Dkt. Ndugulile amesema kuwa Serikali imeboresha vituo vya afya zaidi ya 300, ambavyo vitatoa huduma za dharura za upasuaji wakumtoa mtoto tumboni, na hospitali za wilaya 67, katika Mkoa wa Mtwara hospitali za wilaya 3 zinaenda kujengwa, ili kupunguza mzigo katika hospitali za mikoa,
Aidha, DKt. Ndugulile amesema kuwa amesema kuwa kutokana na Hospitali hiyo kuwa na Changamoto za x-ray na gari la kubebea Wagonjwa, Serikali imeahidi kuzitatua changamoto hizo kwa muda mfupi ili wananchi wa Mtwara waanze kupata huduma hizo mara moja.
"Mmeongelea huduma za mionzi (x-ray), niwaahidi tutawaletea mashine mpya ya x-ray za kidigitali, lakini vile vile kama kuna changamoto ya gari la kubebea wagonjwa, zikija tutazigawa, tunataka hospitali za mikoa zianze kuonekana kwamba ni hospitali za mikoa kweli" alisema Dkt. Ndugulile
Mbali na hayo Dkt. Ndugulile amesema kuwa Serikali inatambua pengo la watumishi katika sekta ya afya, hivyo mwaka uliopita iliweza kuajiri watumishi takribani 11,000, huku watumishi 3000 kuziba pengo la watumishi ambao hawakuwa na vigezo, na 8000 walikuwa ni ajira mpya.
"Tumeweza kuajiri Watumishi takribani 11,000, 3000 kuziba pengo la watumishi ambao hawakuwa na vigezo na vyeti, na ajira mpya ni 8000, kuwahiyo jumla watumishi 11, kadri tunavoendelea kupata uwezo tutaendelea kuongeza rasilimali watu kuhakikisha kwamba tunaziba mapengo yaliyopo" alisema DKt. Ndugulile.
No comments:
Post a Comment