ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, March 16, 2019

JAJI SAMMATA AWAASA WANASHERIA KUKEMEA RUSHWA NA KUWA WAAMINIFU KATIKA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YAO


 Jaji Mkuu mstaafu na Mkuu wa chuo kikuu cha Mzumbe Barnabas Sammata akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha sheria nchini katika mdahalo wa uwajibikaji na mapambano dhidi ya rushwa katika utoaji wa huduma ya haki na mahakama na amewaasa wanasheria hao kuwa mstari wa mbele katika kukemea vitendo hivyo, leo jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya WAJIBU na Mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za Seeikali (CAG) Mstaafu Ludovick Utouh akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha sheria nchini katika mdahalo wa uwajibikaji na mapambano dhidi ya rushwa katika utoaji wa huduma ya haki na mahakama, Leo jijini Dar es salaam.
 Makamu mkuu wa chuo cha Sheria nchini Dkt. Luqman Zakayo akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha sheria nchini katika mdahalo wa uwajibikaji na mapambano dhidi ya rushwa katika utoaji wa huduma ya haki na mahakama,na ameishukuru taasisi ya WAJIBU kwa kuendelea kuandaa viongozi wa baadae kupitia midahalo ya namna hiyo, leo jijini Dar es Salaam.
   Jaji Mkuu mstaafu na Mkuu wa chuo kikuu cha Mzumbe Barnabas Sammata(kushoto) akimkabidhi zawadi ya vitabu Makamu mkuu wa chuo cha Sheria nchini Dkt. Luqman Zakayo(kulia) wakati wa mdahalo wa uwajibikaji na mapambano dhidi ya rushwa katika utoaji wa huduma ya haki na mahakama,na ameishukuru taasisi ya WAJIBU kwa kuendelea kuandaa viongozi wa baadae kupitia midahalo ya namna hiyo, leo jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya WAJIBU na Mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za Seeikali (CAG) Mstaafu Ludovick Utouh.
 Mwakilishi wa taasisi ya TWAWEZA Anastazia Lugaba  akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha sheria nchini katika mdahalo wa uwajibikaji na mapambano dhidi ya rushwa katika utoaji wa huduma ya haki na mahakama, ambapo amesema kuwa mapambano dhidi ya rushwa ni ya wote na amewataka wanasheria hao kuhudumia wananchi kwa haki na usawa  leo jijini Dar es salaam.
 Baadhi ya wanafunzi wa chuo cha sheria nchini wakichangia mada na kuuliza maswali katika mjadala huo uliolenga kujadili mapambano dhidi ya rushwa katika utoaji wa huduma za haki na mahakama, leo jijini Dar es Salaam.
 Sehemu ya washiriki waliohudhuria mdahalo huo ambao ni wanafunzi wa chuo cha sheria nchini wakifuatilia mjadala huo uliohusu  Mapambano ya rushwa katika utoaji wa huduma ya haki na mahakama, leo jijini Dar es Salaam.
Picha ya pamoja



*Awataka kuwa mstari wa mbele kukemea rushwa na kuwa wawajibikaji

* Mkurugenzi wa WAJIBU ampongeza Rais Magufuli katika ufuatiliaji na utekelezaji

Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
TAASISI ya WAJIBU inayojishughulisha na fikra ya uwajibikaji wa Umma leo Machi 16 imefanya mdahalo mkubwa uliokuwa na mada ya Mapambano dhidi ya rushwa katika utoaji wa huduma na mahakama uliowakutanisha wanafunzi wa sheria kutoka chuo cha sheria nchini pamoja na Jaji mkuu mstaafu Barnabas Sammata wakiongozwa na Mkurugenzi wa taasisi ya WAJIBU na CAG mstaafu Ludovick Utouh pamoja na viongozi kutoka TAKUKURU na Azaki mbalimbali.

Akizungumza katika mdahalo huo na wanafunzi wa chuo cha sheria nchini jaji mkuu mstaafu Barnabas Sammata amesema kuwa kuwepo kwa kansa ya rushwa nchini kunasababishwa na mambo kadhaa ikiwemo kurahisha upatikanaji wa huduma,bidhaa na mapato, kupata usichostahili ili kumuumiza mpinzani, kukwepa kupunguziwa kulipa mapato, kodi au faini pamoja na kupata msaada wa kisheria.


Akieleza madhara ya rushwa Jaji Sammata amesema kuwa kansa hiyo ni kuwanyang'ganya wananchi haki yao hasa matarajio yao ya baadaye ikiwemo maisha bora na maendeleo waliojiwekea, amesema kuwa rushwa  hujenga chuki kwa kuwa huvunja haki na waathirika huchukua sheria mkononi wakiona vyombo husika havijatenda haki.

Jaji Sammata ametoa maoni yake na kusema kuwa ili kuepuka hayo yote lazima elimu zaidi kwa umma itolewe na kushauri vyama vya siasa hasa chama tawala na vyombo vya dola kukemea vitendo hivyo huku akihimiza taasisi za dini zishiriki katika kupinga kampeni hiyo kwa kutoruhusu mapato ya rushwa kutunisha kampeni hizo.

Aidha amewataka wanasheria nchini kote kuwa mstari wa mbele katika kupinga vitendo hivyo na kuwa waaminifu kwani rushwa bila kujali ukubwa au udogo wake zinaathiri maendeleo ya jamii huku akisisitiza watakaokiuka taratibu za kisheria kuchukuliwa hatua kali kwa watakaokutwa na vitendo vya aina hiyo wakiwemo wanasheria na waandishi wa habari watakaokutwa na hatia dhidi ya rushwa kwani wao ndio ngao muhimu katika kumulika vitendo hivyo.

Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa taasisi WAJIBU Ludovick Utouh amesema kuwa taasisi hiyo ni changa na alianzisha baada ya kuona uwajibikaji haukuwa imara na hakukuwa na ushirikishwaji wa wananchi moja kwa moja.

Ameeleza kuwa amefurahishwa na kazi ya Rais Dkt. John Joseph Magufuli kwa kuangalia kwa umakini suala la wabunge kuwa wajumbe wa bodi za mashirika mbalimbali hali inayoleta mgongano wa kimaslahi, Utouh amesema kuwa suala hilo amepambana nalo alipokuwa mkaguzi na mdhibiti wa hesabu za serikali (CAG) lakini wengi hawakumwelewa ila Rais Magufuli amelitendea kazi mara tu baada ya kuingia madarakani.

Pia Kaimu mkuu wa Chuo cha Sheria nchini Dkt Luqman Zakayo amesema kuwa mada hiyo ni muhimu sana katika kujenga dhana nzima ya uwajibikaji kwa wanafunzi hao ambao ndio viongozi wa kesho na amewashukuru wanafunzi waliojitokeza katika mjadala huo.

Aidha amemshukuru jaji mkuu mstaafu Barnabas Sammata kwa kuwatengeneza vijana wengine wengi wanaofuata nyayo zake hasa katika kuwarithisha vijana hao mambo mazuri yanayozidi kujengwa miongoni mwao.

Vilevile ameipongeza taasisi wa WAJIBU kwa shughuli wanazozifanya ambazo kwa ukubwa wake zinagusa kila sekta katika jamii.

No comments: