ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, March 27, 2019

Meya wa Manispaa ya Mtwara Mikindani Na Diwan Mmoja Watangaza Kuhamia CCM Wakitokea CUF


Na Bakari Chijumba, Mtwara.
Meya wa Manispaa ya Mtwara Mikindani ambaye pia ni Diwani wa kata ya Tandika,Geoffrey Isack Mwachisye ametangaza rasmi kujiunga na chama cha Mapinduzi(CCM) akitokea Chama cha wananchi (CUf).



Mwanchisye ametangaza uamuzi huo hii Leo 27 March 2019 kwenye ofisi za Chama cha mapinduzi Wilaya ya Mtwara,mbele ya Katibu wa CCM Mkoa El-Haj Kusilawi na viongozi wengine wa chama cha mapinduzi wilaya.

"Kimsingi nimeamua kuungana na chama cha mapinduzi ili kuunga mkono juhudi za Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hakuna ambaye ametutishia wala kutupa fedha" amesema Mwanchisye na kuongeza kuwa;

"Mimi kama Meya nilikua napambana kutekeleza majukumu lakini Combination ya timu niliyotoka haikua nzuri, tumeona kuna kila haja ya kurudi kwa kocha mahiri ambaye ni Rais Magufuli, nitakuwa muaminifu wa chama na kwa nchi yangu"

Aidha Meya Mwanchisye ameambatana na diwani wa Kata ya Chikongola (CUF), Musa Namtema (Fasheni) ambaye naye amejiunga na CCM huku akitoa sababu ya kwamba anaamini CCM ni chama ambacho kitawawezesha kuwatumikia wananchi vizuri kwa kutekeleza ilani ya chama kilicho madarakani.

Kabla ya kutimkia CCM Meya Mwanchisye amewahi kutajwa kutofautiana na viongozi waandamizi wa Chama chake cha awali (CUF), ngazi ya wilaya, baada ya kusimamia upitishwaji wa sheria ndogo ya ongezeko la Kodi ya mabanda ya biashara kulikopelekea wafanyabiashara mjini Mtwara kugoma.

No comments: