ANGALIA LIVE NEWS

Monday, March 25, 2019

WAZIRI KAMWELWE AWATAKA WATUMISHI SEKTA YA UJENZI KUONGEZA UBUNIFU

 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe, akikaribishwa na Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Sekta ya Ujenzi, Arch. Elius Mwakalinga, alipowasili kufungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi, mjini Dodoma. Kulia ni Katibu wa Baraza hilo, Wakili Fanuel Muhoza.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, akisalimiana na Mkurugenzi wa Sera na Mipango kutoka Sekta ya Ujenzi, Bi. Elizabeth Tagora, kabla ya kufungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Sekta hiyo, mjini Dodoma.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi wa Sekta hiyo, Arch. Elius Mwakalinga (wa pili kushoto), akiongoza wimbo wa mshikamano daima katika kikao cha Baraza la Wafanyakazi kilichofanyika mjini Dodoma.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe, akisisitiza jambo kwa wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Sekta ya Ujenzi (hawapo pichani), wakati akihutubia Baraza hilo mjini Dodoma.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi wa Sekta hiyo, Arch. Elius Mwakalinga, akihutubia wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Sekta hiyo (hawapo pichani), katika kikao cha Baraza la Wafanyakazi mjini Dodoma.
 Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi kutoka Sekta ya Ujenzi wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi katika kikao cha Baraza hilo, kilichofanyika mjini Dodoma.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi kutoka Sekta ya Ujenzi, mjini Dodoma.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, amewataka wafanyakazi wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), kuongeza ubunifu na bidii katika kazi wanazozifanya ili kuendana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia yanayoendelea duniani.
Mhandisi Kamwelwe, amesema kuanzia sasa wafanyakazi wa sekta hiyo wawekewe mkakati utakaowapa fursa za kutosha kujiendeleza kitaaluma ili kuwezesha Wizara na Taifa kuwa na wataalam wakutosha wenye ubunifu wa kisasa na hivyo kuhakikisha miradi inayosimamiwa na Serikali inakuwa yenye ubora.

Akifungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Wizara yake mjini Dodoma Mhandisi Kamwelwe amehimiza umuhimu wa kila mfanyakazi katika Wizara hiyo kukabiliana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia katika eneo lake la kazi ili kuhakikisha kazi zinazofanywa zinapimika na kuleta tija.
“Hakikisheni watumishi wanaendelezwa kila wakati ili kukidhi mahitaji ya soko la ajira na mabadiliko ya sayansi na teknolojia yanayotokea sasa duniani kote,” amesisitiza Waziri Kamwelwe.
Amezungumzia umuhimu wa wafanyakazi kusikilizwa na kupewa motisha pale wanapobuni masuala yatakayoisaidia sekta ya ujenzi katika kukuza teknolojia na kuzingatia thamani ya fedha ili kuwezesha nia ya Serikali ya kuwa na wataalam wengi katika miradi mikubwa ya ujenzi nchini kufikiwa.

Naye Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Sekta ya Ujenzi  Arch. Elius Mwakalinga, amewataka wafanyakazi na viongozi katika sehemu za kazi kuhakikisha upendo na mshikamano vinatawala mahali pa kazi wakati wote ili  kuwezesha ubunifu, bidii na tija kufikiwa.
Amemtaka kila mtumishi wa Sekta ya Ujenzi kuwa na malengo ya kazi yanayopimika na kujipima kila wakati ili Wizara ijue changamoto zilizopo na kuzipatia ufumbuzi kwa wakati.

Katika Baraza hilo pamoja na kupitisha makadirio ya bajeti ya sekta ya ujenzi kwa mwaka wa fedha 2019 pia limemchagua Wakili, Fanuel Mhozya kuwa Katibu wa Baraza hilo.

No comments: