Mtaalam wa Sheria Kutoka MKURABITA Jane Lyimo akiongea na waandishi wa Habari Juu ya Mafunzo ya siku Mbili kwa wajasiliamali wa Manispaa ya Mtwara Mikindani kwa lengo la kujiongezea Kipato katika Biashara zao.
Afisa Biashara Manispaa ya Mtwara Mikindani Edward Matulanya akitoa mafunzo juu ya umuhimu wa kurasimisha bishara ili kuweza kutambulika na serikali na umuhimu wa ulipaji wa kodi.
Baadhi ya wajasiliamali kutoka manispaa ya Mtwara Mikindani wakisikiliza kwa Makini Mfunzo yaliyoandaliwa na MKURABITA kwa lengo la kuwajengea uwezo juu kukuza mitaji na kutunza kumbukumbu.
JOSEPH MPANGALA
Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za wanyonge Tanzania MKURABITA kwa kushirikiana na Manispaa ya Mtwara Mikindani,Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA pamoja na taasisi mbalimbali za Kifedha zimetoa mafunzo kwa wajasilimali zaidi ya Elf Moja ili kuweza kujenga uwezo katika kuweka Kumbukumbu za Biashara na kuongeza kipato.
Akiongea katika Ufunguzi wa Mafunzo hayo ya Siku mbili Mtaala wa Sheria Kutoka MKURABITA Jane Lyimo anasema Walianza kwa kufanya tathmini ili kuweza kugundua changamoto za wafanyabiashara wa Mkoa wa Mtwara na kwa kiasi gani wamerasimishwa na kutambulika na serikali.
“Kazi kubwa iliyofanyika ni pamoja na kufanya Tathmini kwa wafanya biashara elf moja nia na madhumuni ni kutaka kujua wafanyabiashara wa manispaa wako katika hali gani,biashara zao zinaendeshwa katika mfumo gani,wako rasmi au hawako rasmi,ni Changamoto gani wanakutana nazo na baada ya kumaliza tathmini ni kuwapeleka katika mafunzo”Amesema Jane Lyimo.
Ameongeza kuwa Tathmini imeonesha kuwa Biashara nyingi Mkoani Mtwara Zinashindwa kukua kutokana na sababau mbali mbali ikiwemo kutunza kumbukumbu za Mauzo pamoja na kujiunga na mifuko ya jamii.
‘’Wafanyabiashara elf moja waliofanyiwa Tathmini ni wafanyabiashara 153 tu ndio ambao wanatunza Kumbukumbu lakini pia Wafanyabiasha Tisa kati ya elf Moja ndio wamejiunga na mifuko ya jamii idadi ambayo ni ndogo na wengi wa wafanyabiashara hawatunzi fedha zao katika Taasisi za Kifedha hii inapelekea mitaji yao kushindwa kukua kutokana na Kutokuwa na Uhusiano katika Taasisi za Kifedha”
Zaidi ya wajasiliamali 1000 wameshiriki katika Mafunzo ya kuwajengea uwezo juu ya Kurasimisha biashara zao pamoja Elim ya ulipaji wa Kodi.
No comments:
Post a Comment