ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, April 23, 2019

Mnazi Mmoja yaichabanga Muhimbili 40-16 katika mpira wa pete

 Kikosi cha timu ya mpira wa pete kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili wakifanya mazoezi kabla ya mchezo huo kuanza.
 Mchezaji wa Timu ya Muhimbili Nzitu Msengi (WD) akitoa pasi kwa Kuruthum (c ) katika mchezo uliofanyika kwenye kiwanja cha Gymkhana
 Julieth Jabu (GA) akiifungia timu ya Muhimbili goli la nane katika mchezo huo.
 Baadhi ya washabiki wa mpira wa pete wakifuatilia mechi kati ya Muhimbili na Mnazi Mmoja.


Timu ya mpira wa pete ya Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar imeibuka mshindi baada ya kuichabanga Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) bao 40-16 kwenye michezo ya Bonanza la Pasaka inayoendelea mjini humo.

Katika mchezo huo uliofanyika uwanja cha Gymkhana Zanzibar hadi kipindi cha kwanza kinaisha timu ya Mnazi Mmoja iliongoza kwa bao 16-5. Mara baada ya mchuano huo kuisha nahodha wa timu ya Hospitali ya Mnazi Mmoja, Maneno Shaame amesema mtangane huo ulikuwa mzuri na ushindi wao umetokana timu yake kufanya mazoezi ya kutosha na hivyo kujiandaa kikamilifu.

“Tunashukuru tumecheza vizuri na mpaka sasa hivi timu tunaijenga ili kufikia mafanikio mazuri zaidi kwa michezo ijayo” amesema Shaame. Naye kocha wa timu ya Muhimbili Zainabu Kassim amekiri kuwa kufungwa kwa timu yake kumetokana na makosa waliyofanya wakati mchezo huo ukiendelea hivyo wamejifunza na kwamba wataijenga zaidi timu hii.

“Mchezo ulikuwa mzuri na hivyo kwa kuwa tunaijenga timu yetu, tumejua tuko wapi na tunaelekea wapi, changamoto tumeiona japo tumefungwa lakini tumejifunza,” amesema Zainabu Bonanza la Michezo ya Pasaka linaendelea Zanzibar kati ya Hospitali ya Taifa Muhimbili na Hospitali ya Mnazi Mmoja ambalo linajumuisha mpira wa miguu na pete.

No comments: