Naibu meya
wa manispaa Joseph Lyata ya Iringa akiwa na
msanii Rehebian Kigahe aliyekua anazindua albam inayoitwa “wema na fadhili za bwana”katika kanisa la PHM Mkwawa
Msanii Rehebian Kigahe akiongea neno wakati wa kuzindua albamu yake ya “wema na fadhili za bwana” katika kanisa la PHM Mkwawa
Baadhi ya waumini na mashabiki wa msanii Rehebian Kigahe waliohudhulia katika uzinduzi wa albamu ya msanii huyo
NA
FREDY MGUNDA,IRINGA.
NAIBU meya wa manispaa ya Iringa
amewataka waumini na wananchi kote nchini kuendelea kuliombea taifa kudumisha
amani na upendo uliopo ili kuepukana na machafuko kama ilivyo kwenye nchi
nyingine za jirani.
Akizungumza wakati wa uzinduzi
wa album ya msanii Rehebian Kigahe inayoitwa “wema na fadhili za bwana” Naibu meya
wa manispaa Joseph Lyata alisema, kupitia makanisa na madhehebu mengi kuendelea
kuhubili ambani kokote kule ambako wanauwezo kuwafakia wananchi.
“Leo tunazindua album hii ya “wema
na fadhili za bwana” imetuunganisha watu wote kuongea lugha moja na kuendelea
kutunza amani yetu hivyo niwaombe wananchi nao waendelee kuhubili amani”
alisema Lyata
Lyata alimpongea msanii aitwaye
Rehebian Kigahe kwa kuandaa albam ambayo imebeba ujumbe wa kumuabudu na kumsifu
mwenyezi mungu jambo linalopelekea watanzania nao kuiga mfano wa msanii huyu
kusisitiza amani iliyopo
“Naomba kwa dhati yangu kumpongeza msanii huyu kwa kazi nzuri ya
kumpongeza msanii huyu kwa kutunga nyimbo za kumwabudu mwenyezi mungu kwa kuwa
ujumbe wake utaenea nchi nzima kwa kutumia nyimbo zake”alisema Lyata
Aidha Lyata aliwaomba
watanzania kuinunua albu ya msanii Rehebian Kigahe kwa kuwa imejaa nyimbo za
kumsifu bwana na zenye mafunzo mengi kwa jamii huku lengo likiwa kuwasaidia na
kuwainua wasanii kama Rehebian Kigahe ambao bado hawajajulikana hivyo.
“Albam hii mimi nimeipenda na
nimesikiliza nyimbo zake zinaujumbe mzuri sana,ningependa kila mtanzania aipate
albam hii kwa kuwa ujumbe wake unatufanya tuendelee kumwabudu mwenyezi mungu”
alisema Lyata
Kwa upande wake msanii wa
nyimbo hizo za injili Rehebian Kigahe alimshukuru Naibu meya wa manispaa ya Iringa
kwa ujumbe wake kwa taifa juu ya albam yake na kuwaomba watanzania wamuunge
mkono ili aweze kuwahubilia wananchi kwa kutumia uimbaji.
Namshukuru mungu leo nimezindua
albam yangu ambayo inanyimbo tisa na albam hii inaitwa “wema na fadhili za
bwana” ambayo nauhakika wa kuwa atakayesikiza albam hii atapata wokovu mzuri
kwa ujumbe ambao nimeukalisha kwa njia ya nyimbo hizi” alisema Kigahe
Kigahe aliwaomba watanzania
kuitafuta na kuinunua albamu hiyo ya “wema na fadhili za bwana” kwa kuwa
inamafunzo mengi sana yaliyopo ndani ya nyimbo zilizopo humo ndani
No comments:
Post a Comment