Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi(Mb.),(kulia) akiwa katika mazungumzo na Naibu Msaidizi wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki na Sudan, Balozi Makila James, katika Ofisi ndogo za Wizara Dar es salaam leo tarehe 30 Aprili, 2019.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi(Mb.), akimuonesha Naibu Msaidizi wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki na Sudan, Balozi Makila James (katikati) maeneo mbalimabali katika ramani alipokuwa akielezea historia ya Tanzania.Kushoto kwake ni kaimu Balozi wa Marekani Mhe. Imni Patterson.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe.Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) akimuelezea Naibu Msaidizi wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki na Sudan, Balozi Makila James kuhusu uhuru wa vyombo vya habari nchini Kushoto kwake ni Kaimu Balozi wa Marekani nchini, Mhe. Imni Patterson.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini (DGCU), cha Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Emmanuel Buhohela (wa kwanza kulia) na Afisa Mambo ya Nje wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Albert Philipo, wakifuatilia mazungumzo baina ya Mhe. Prof Palamagamba John Kabudi na Balozi Makila James.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Palamagamba John Kabudi(Mb.) akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Msaidizi wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki na Sudan, Balozi Makila James (wa pili kushoto), kulia kwake ni Kaimu Balozi wa Marekani nchini, Mhe. Imni Patterson. Wengine ni afisa wa Wizara wa Mambo ya Nje, Albert Philipo (wa kwanza kulia) na afisa wa Uchumi katika ubalozi wa Marekani nchini Ann Marie Warmenhoven (wa kwanza kushoto).
No comments:
Post a Comment