ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, April 30, 2019

Schreiber asisitiza Tanzania kutosaini mkataba wa EPA

Mbunge na Mwenyekiti wa Kamati inayohusika na Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo ya Ujerumani Mhe. Eva-Maria Schreiber amefanya ziara ya siku saba hapa nchini Schreiber amepata fursa ya kutembelea mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma na Kigoma, ambapo pia amekutana na wenyeviti wa Kamati mbalimbali za Bunge.

Akiwa nchini Mbunge huyo ametembelea mradi wa maji ujulikanao kama “Seven Towns Urban Upgrading Programme/ Kigoma Urban Water Supply and Sanitation”. Mradi unafadhiliwa na Umoja wa Ulaya na Serikali ya Ujerumani kupitia Benki ya Maendeleo ya Ujerumani (KfW). 

Aidha, mradi huo unahusisha mikoa ya Kigoma, Shinyanga na Lindi. Kwa upande wa Kigoma, utekelezaji wa mradi huu ulianza mwezi Machi 2013 na utakamilika mwezi Oktoba, 2019.Mhe. Schreiber amekutana na kufanya mazungumzo na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam. Katika mazungumzo hayo na waandishi wa habari Mhe. Schreiber amesisitiza umuhimu wa Tanzania kutokusaini Mkataba wa Makubaliano ya Kuichumi (EPA) kati ya Jumuiya ya Umoja wa Ulaya na nchi za Afrika.

Pia alieleza kuwa endapo Tanzania na nchi nyingine za Afrika hazitofaidika na Mkataba huo kwakuwa zitapoteza mapato. 
Sehemu ya waandishi wakimsikiliza kwa makini Mhe. Schreiber.
Schreiber akiendelea kuzungumza na waandishi wa Habari. 

No comments: