Balozi wa Tanzania nchini Urusi, Mhe. Maj. Jen. Mstaafu Simon Mumwi akitoa neno la ukaribisho kwa wageni mbalimbali walioalikwa kushiriki kilele cha kuadhimisha Siku ya Taifa ya Tanzania (Maadhimisho ya miaka 55 ya Muungano) yaliyofanyika jijini Moscow tarehe 26 Aprili 2019. Maadhimisho hayo yalipambwa na shughuli mbalimbali zikiwemo Maonesho ya bidhaa na vivutio vya utalii vya Tanzania; kukabidhi vyeti kwa wadau mbalimbali ili kutambua mchango wao katika maendeleo ya uchumi wa Tanzania, hususan katika sekta ya utalii, uwekezaji, sanaa, lugha na utamaduni pamoja na kutoa fursa ya kubadilishana mawazo baina ya Mabalozi na taasisi za Urusi zinazojihusisha na masuala ya uwekezaji. Mwingine katika picha ni Naibu Mkurugenzi wa Afrika kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi, Bw. George Cherpisk.
Naibu Mkurugenzi wa Afrika kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi, Bw. George Cherpisk akisoma hotuba katika maadhimisho hayo.
Mhe. Balozi Mumwi na Waheshimiwa Mabalozi wa mbalimbali wa nchi za Afrika zenye uwakilishi nchini Urusi wakikata keki ya kuadhimisha miaka 55 ya Muungano wa Tanzania.
Balozi wa Tanzania nchini Urusi, Mhe. Maj. Jen. Mstaafu Simon Mumwi akikabidhi cheti kwa mmoja wa wadau wanaochangia maendeleo na ukuaji wa uchumi nchini Tanzania.
Mdau akipokea cheti chake ikiwa ni ishara ya kutambua mchango wake katika maendeleo ya Tanzania.
Picha ya pamoja ya baadhi ya Waheshimiwa Mabalozi, wageni, maafisa wa ubalozi na wanafunzi wa Kitanzania wanaosoma Urusi walioshiriki katika maadhimisho hayo.
No comments:
Post a Comment