Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akikata utepe kuashiria uwashaji rasmi wa umeme katika kijiji cha Changarawe, wilayani Songea, Mkoa wa Ruvuma, Aprili 3, 2019 akiwa katika ziara ya kazi.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (kushoto), akikabidhi kifaa cha Umeme Tayari (UMETA) kwa wananchi wa kijiji cha Changarawe, wilayani Songea, Mkoa wa Ruvuma baada ya kuwasha rasmi umeme katika kijiji hicho Aprili 3, 2019.
Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani (wa pili-kulia), akiwa katika ziara ya kazi kukagua utekelezaji wa miradi ya umeme katika kijiji cha Changarawe, wilayani Songea, Aprili 3, 2019. Waziri aliwasha rasmi umeme katika kijiji hicho. Wengine pichani ni viongozi na wataalamu mbalimbali kutoka wizarani, TANESCO na REA.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (wa pili – kulia), akizungumza na wananchi wa kijiji cha Unangwa, wilayani Songea, alipofika kuwawashia rasmi umeme, Aprili 3, 2019 akiwa katika ziara ya kazi.
No comments:
Post a Comment