ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, April 18, 2019

WIZARA YA AFYA IDARA KUU MAENDELEO YA JAMII YAANZA KAZI RASMI MJI WA SERIKALI

 Katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu akifurahia jambo mara baada kuanza kazi Makao Makuu Mapya ya Wizara yake yaliyoko eneo la Mtumba nje kidogo ya Jiji Dodoma.
 Mkurugenzi wa Idara ya Watoto Mwajuma Magwiza wa Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii mara ya kuanza majukumu yake katika Ofisi Mpya zilizoko Mtumba nje Kidogo ya Jiji la Dodoma.
Mkurugenzi wa Idara Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Leornard Mchau mara ya baada kuanza majukumu yake katika Ofisi Mpya zilizoko Mtumba nje Kidogo ya Jiji la Dodoma.

Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii imeanza rasmi kutoa huduma za Ofisi katika mji wa Serikali uliopo Mtumba nje kidogo ya Jiji la Dodoma na kuwataka wananchi kufuata huduma za kiofisi katika ofisi hizo mpya. .

atibu Mkuu wa Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu amesema kimsingi Ofisi yake kwa sasa inatoa huduma zake katika ofisi zake zilizoko Mtumba na kuwataka wateja wake kufuata huduma hapo ambazo zitakuwa wazi muda wote

"Nawakaribisha sana wananchi wote kuanza kutumia ofisi zetu hapa eneo la Mtumba na tuko hapa kama hatua muhimu ya kutekeleza kikamilifu agizo la Rais kwa vitendo." Aliongeza Dkt.Jingu. .

Aidha, Mkurugenzi wa Utawala na Wizara na Rasilimali Watu Leornad Mchau amesema ni uamuzi muhimu sana wa kuweka Ofisi za Serikali mahali pamoja ili wananchi waweze kupata huduma hizo kwa haraka na kwa gharama nafuu. .

Ameusifu uamuzi wa Serikali kuwa wa msingi sana akitofautisha na Dar es Salaam ambapo Wizara za Serikali zilitapakaa maeneo mbalimbali ya Jiji lakini kwa sasa hata kama ukitokea Jijini Dar es Salaam ni rahisi kupata huduma za Serikali katika eneo moja.

Wakati huohuo Mkurugenzi wa Idara ya Watoto kutoka Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Mwajuma Magwiza ametoa rai kwa uongozi wa Jiji la Dodoma kuharakisha miundombinu ya usafiri ili wananchi wanaoitaji huduma za kiofisi waweze kufika katika eneo la Mtumba na kupata huduma hiyo kwa haraka.

Magwiza ameongeza kuwa kwa maoni yake wateja watu wanahitaji miundombinu rafiki ili waweze kuhudumiwa na ofisi yake kwa haraka lakini ana imani uongozi wa Jiji utaharakisha au kulifanyia kazi jambo hili na kuwezesha wananchi kupata huduma ya haraka na kuwataka kuweka tayari mipango miji ili wawekezaji waweze kuwekeza jilani na eneo hilo.

Wizara za Serikali tayari zimeanza kutolewa katika Jiji jipya la Serikali kufuatia agizo la Mhe. Rais la kuwataka Viongozi wa Setikali kuanza kutoa huduma zao Mtumba baada ya kukamilika kwa Ofisi hizo.

No comments: