Katibu Mkuu wa AWFISHNET, Bi. Editrudith Lukanga akizungumza kwenye mkutano huo wa kwanza uliofanyika leo Aprili 18,2019, Jijini Dar es Salaam.
MTANDAO wa
Wanawake wa Afrika wanaojihusisha na shughuli za uvuvi, uchakataji wa samaki na
mazao yake (African Women Fish
Processors and Traders Network- AWFISHET)
kutoka nchi 28 za Afrika wamekutana Jijini Dar es Salaam katika mkutano
Mkuu wa kwanza wa mwaka kujadiliana
namna ya kutatua changamoto za masoko na namna ya kuendeleza shughuli zao.
Awali
akifungua mkutano huo, Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina uliofunguliwa
kwa niaba yake na Bi. Flora Luhanga kutoka wizara hiyo aliwataka Wanawake wa Afrika kuwa kitu kimoja haswa
katika utungaji wa sera zenye kuwajenga na zenye kuwaweka kwenye njia sahihi za
maendeleo.
Waziri Mpina
aliwataka wanawake hao kuwa kioo kwa wengine pindi watakaporejea kwenye nchi
zao kwani anahakika mijadala na mambo
mbalimbali waliojifunza kwenye mkutano huo ni ishara tosha kuwa kwa sasa
wanafikia malengo yao kama wanawake katika sekta ya uvuvi Bara la Afrika.
Nae Rais wa
AWFISHNET, Bi. Beyeue Ateba Baliaba amewataka Wanawake hao kuendelea kuwa kitu
kimoja na kuleta kwa pamoja mawazo yao ili yaweze kutatuliwa kwa sauti moja.
Kwa upande
wake Katibu Mkuu wa AWFISHNET, Bi. Editrudith Lukanga amewataka Wanawake wa Afrika kushiriki
kikamilifu kwani mkutamo huo utajadili mkakati wa nmna ya kushughulikia
changamoto kwenye nchi zao na namna ya kuzitatua.
“Mkutano huu
wa siku mbili, unashirikisha wajumbe zaidi ya 60, kutoka nchi 28 za Bara la
Afrika hasa Wanawake wanaojihusisha na shughuli za uvuvi.
Leo kila
mjumbe amewasilisha mada na namna ya shughuli anazofanya nchini mwake ili kuona
tunafikia malengo yetu kwa pamoja ikiwemo namna ya kutafuta na kupata mitaji,
masoko, miundombinu ya uchakataji na mambo mengine yanayofanana na hayo.” Alisema
Bi. Editrudith Lukanga.
Bi. Editrudith
Lukanga aliongeza kuwa, mkutano huo,
wajumbe wataweza kushiriki katika maasuala mbalimbali yakiwemo utengenezaji
sera, sheria, kanuni pamoja na utekelezaji wake kama msingi mkubwa wa kuwezesha
sekta kuwa endelevu na pia kuchangia kwenye lishe na usalama wa chakula.
Aidha,
amewashukuru wadau waliowezesha mkutano huo wa mwaka na wa kwanza kwa mafanikio
makubwa huku akiendelea kuwaomba waendelee kuwasapoti zaidi.
“Mwanamke ni
kiungo cha jamii, kwani ukimsapoti mwanamke, umesapoti jamii nzima katika
kupambana na umasikini. Uwepo wetu hapa
umewezeshwa na sie pamoja na wadau wetu. Natoa wito kwa Serikali zote wanakotoka Wanachama wetu waweze kuweka
mikakati ya makusudi ya kuwatambua kazi
zao na kuweza kuwasaidia.
AWFISHNET
imeanzishwa mnamo Aprili 17, 2017 huku ikiwa na wajumbe kwenye jumuiya za
Kitaifa za wanawake wanajishughulisha na uvvuvi katika nchi zao. Katika mkutano
huo wajumbe washiriki zaidi ya 60, Nchi
za Afrika ikiwemo Tanzania, Zambia, Uganda, Tunisia, Togo, Tanzania, Sudani
Kusini, Sierra Leone, Senegal, Nigeria, Mauritania, Mali, Malawi, Madagascar,
Liberia, Kenya.
Baadhi ya Wajumbe wakiwa kwenye mkutano huo
Makamu wa Rais wa AWFISHNET, Bi.Jeriedayaro Uwhraka akizungumza kwenye tukio hilo
Mwakilishi Shirika la Chakula Duniani (FAO) kwa Afrika, Martin Van Der Knaap akizungumza kwenye mkutano huo wakati wa ufunguzi
Bi. Flora Luhanga akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo kwa niaba ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina.
Katibu Mkuu wa AWFISHNET, Bi. Editrudith Lukanga akizungumza kwenye mkutano huo wa kwanza uliofanyika leo Aprili 18,2019, Jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment