ANGALIA LIVE NEWS

Friday, May 31, 2019

KAMPUNI YA GREEN WASTE PRO YAWEKA MAPIPA YA KUKUSANYIA MIFUKO YA PLASTIKI KWENYE MIJI YA DAR,DODOMA NA MWANZA


 Meneja wa Green Waste Pro tawi la Dodoma, Abdalla Mbena akizungumza katika tukio.


KAMPUNI ya Green Waste Pro (GWP)  kwa kushirikiana na Halmashauri za Miji ikiwemo ya Dar es Salaam, Dodoma na Mwanza  wamekuja na mkakati maalum ya kukusanya mifuko ya plastiki katika kuunga mkono juhudi za Serikali kutokomeza matumizi ya mifuko zoezi lililoanza toka Mei 25, mwaka huu.
  
Akizungumza Meneja wa Green Waste Pro tawi la Dodoma, Abdalla Mbena  katika mkutano uliandaliwa na Shirika la ForumCC kwa kushirikiana na Halmashauri ya Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam  ambapo amebainisha kuwa,  tayari wamesambaza mapipa zaidi 60 kwenye miji ya Dodoma, Mwanza na Dar es aSalaam katika Manispaa ya Ilala.
 
“Kwa kuunga juhudiz zoezi la kutokomeza mifuko ya plastiki ‘rambo’ sisi kama Green Waste Pro, tumeweza kusambaza mapipa hayo karibu kila eneo tulilotenga na wananchi wataweza kukusanya mifuko hiyo hapo.

Ili kuweka mazingira rahisi ya kutekeleza agizo hilo la Serikali la katazo la matumizi ya mifuko hiyo zoezi litakaloanza Juni Mosi mwaka huu.” Alisema Mbena.

Mbena ameonegza kuwa, wananchi wametakiwa kupeleka mifuko hiyo kwenye vituo hivyo  vya kukusanyia pamoja na maeneo mengine yaliyotengwa na Serikali.

Green Waste Pro wameweka mapipa hayo kwa Halmashauri Ilala katikati  eneo la Kaburi moja Mitaa ya Samora, Jamhuri na Libya huku pia wakiweka katika maeneo mengine ya katikati katika miji ya Dodoma na Mwanza.
 
Mwisho Mbena amewataka wananchi kuchangamkia nafasi hiyo na kuiwakilisha mifuko hiyo kabla ya kuanza kutozwa faini.

Katika tukio wamewakutanisha wadau mbalimbali wakiwemo wakandarasi wa kubeba taka ngumu kwa lengo la kujadili changamoto za kimazingira na kutafuta ufumbuzi wake.

Mjadala huo unafanyika chini ya ufadhili wa Umoja wa Ulaya(EU) kupitia Mradi wa Mazingira na Mabadiliko ya Tabianchi.
EU wamekuwa wakishirikiana kuandaa mijadala na makongamano yanayohusu kujadili mabadiliko ya tabianchini na hali ya mazingira nchini kwa ujumla.

Awali akizungumza wakati wa ufunguzi wa  majadiliano kwa niaba ya Meya wa Ilala, Naibu Meya wa manispaa hiyo Omari Kumbilamoto alisema ni jambo muhimu wadau kukutana na kuweka mikakati itakayosaidia kuweka mazingira safi hasa kwa kuzingatia Serikali imetangaza kuanzia Juni 1,mwaka huu ni marufuku kwa mtu yoyote kuzalisha, kuingia au kutumia mifuko ya plastiki.

Alisema Ilala ni ndio inayobeba taswira ya nchi na hivyo lazma izingatie kwamba inalo jukumu la kuweka mikakati kwa kushirikiana na wadau wa mazingira kuweka mazingira safi yakiwamo ya kuondoa taka ngumu

Mwandishi wa Habari  hii ni Mjumbe wa Bodi ya Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira (JET),

No comments: