ANGALIA LIVE NEWS

Monday, July 22, 2019

INJINIA MELI YA MV MAPINDUZI AJINYONGA AKIWA SAFARINI

INJINIA msaidizi wa Meli ya MV Mapinduzi inayofanya safari zake Unguja na Pemba, Haji Abdalah Khatib, amekutwa amejinyonga wakati meli hiyo ikiwa safarini kutoka Unguja kwenda Pemba, Kamanda wa Polisi Mjini Magharibi, Thobias Sedeyoka, amethibitisha. Kwa sasa meli hiyo imekatisha safari yake na kurejea Unguja kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Mkurugenzi wa Shirika la Meli na Uwakala Zanzibar, Salum Ahmada Vuai, amethibitisha kutokea kwa kifo hicho ambapo ameeleza kuwa mtu huyo alikuwa kwenye chumba cha mashine na alikuwa peke yake.

”Ni kweli amejinyonga lakini ni mapema sana kujua chanzo lakini meli imelazimika kukatisha safari yake na kurejea Unguja kwa ajili ya uchunguzi zaidi”, amesema Vuai.

”Bado tunaongea na mamlaka husika ili kujua, lakini tu kama mnavyofahamu, leo ni Jumatatu watu wanakwenda kwenye shughuli zao huo Pemba lakini sasa wanarudi Unguja ili tuupate mwili na tufanye uchunguzi kisha tutawajulisha zaidi,” ameeleza. GPL

No comments: