MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, jana Julai 17, 2019, amezindua soko la Kimataifa la Madini na Vito jijini Dar es Salaam ikiwa utekelezaji wa agizo alilotoa Rais John Magufuli kutaka kila mkoa kuwa na soko hilo.
Makonda amesema uwepo wa soko hilo litasaidia wananchi kununua madini na vito halali na kupunguza matapeli waliokuwa wakiuwazia wananchi na wageni madini na vito feki.
Aidha amesema uzinduzi wa soko hilo umekuja wakati muafaka ambao Tanzania imechaguliwa kuwa mwenyeji wamMkutano wa wakuu wa nchi za Jumuia ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) ambao wataingia nchini mwezi ujao wakiambatana na wafanyabiashara ambapo pia anaamini watapata nafasi ya kutembelea soko hilo.
Hata hivyo, amesema ndani ya soko hilo yanapatikana madini ya aina zote, hivyo amewataka wananchi kulitumia kwa kuwa ni halali na linatambulika na serikali.
Mkoa wa Dar es Salaam ndiyo soko na lango kuu la madini, hivyo uwepo wa soko hili ni fursa kwa wachimbaji, wafanyabiashara na wananchi kupata madini na vito halali kwa bei halali.
Imeandaliwa na Neema Adrian/GPL
No comments:
Post a Comment