Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo akikagua moja ya vyumba vya maabara katika shule hiyo mpya iliyopo kata ya Olasiti mkoani hapa. Shule hiyo itaanza kudahili wanafunzi kuanzia januari mwakani 2020.
Msingi wa nyumba za Waalimu katika Shule mpya ya Sekondari ya Mrisho Gambo kama ubavyoonekana katika picha.
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akimkabidhi Afisa Tarafa Mabati mara baada ya kuyapokea.
Diwani wa Kata ya Olasiti Mhe. Alex Marti akizungumza na wasndishi wa habari katiks eneo la shule mpya ya Sekondari ya Mrisho Gambo.
Afisa Tarafa ya Elerai Bw.Titho Maulilyo Cholobi akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhiwa mabati ya kuezekea shule ya sekondari ya Mrisho
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mount Kilimanjaro Safari Club Bw. George Ole Neing'arrai akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhi mabati hayo.
Mkuu wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukagua madarasa pamoja na ujenzi unaoendelea katika shule mpya ya Sekondari ya Mrisho Gambo iliyopo kata ya Olasiti mkoani Arusha.
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo akipokea sehemu ya mabati yenye thaman ya takribani sh. milioni.15 kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mount Kilimanjaro Safari Club George Ole Meing'arrai .
Na Vero Ignatus, Arusha
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo amepokea mabati yenye thamani ya takribani sh. milioni 15 kutoka Kampuni ya Mount Meru Kilimanjaro Safari Club ya Jijini Arusha.
Akizungumza baada ya kupokea mabati hayo amesema mwaka jana 2018 Jiji la Arusha lilipata changamoto kubwa ya wanafunzi zaidi ya 10,000 kukosa madarasa ya kusomea.
Amesema hadi sasa wanajenga madarasa 8 yenye maabara 3 za sayansi, ili kufiklia lengo la kuhakikisha miundombinu ya elimu hususan masomo ya sauansi inakuwepo.
Mhe. Gambo amesema changamoto nyingine ni uhaba wa walimu wa masomo ya sayansi na kwamba tatizo hilo ni kubwa kubwa.
Aidha Afisa ustawi wa jamii Kata ya Olasiti Bi.Victoria Moshi amesema ujenzi wa shule hiyo utasaidia sana katika kipengele cha ulinzi wa ntoto kwani hawataenda umbali mrefu kufuata shule.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mount Kilimanjaro Safari Club amemshukuru mkuu wa mkoa kwa kuwashirikisha kama wakala wa utalii katika maendeleo ya jamii ikiwemo maswala ya Elimu .
Amesema kuwa wataendelea kushirikiana na Serikali katika kuleta maendeleo kwa jamii ambapo ametoa wito kwa taasisi nyingine kuunga mkono juhudi za serikali za kuhakikisha watoto wanapata fursa ya elimu.
No comments:
Post a Comment