Advertisements

Wednesday, July 17, 2019

Prof. Kabudi akutana na Mabalozi wa Nchi za SADC

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) amekutana na kufanya mazungumzo na Mabalozi wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) waliopo hapa nchini.

Katika mazungumzo hayo Prof. Kabudi amewafahamisha hatua iliyofikiwa katika maandalizi ya Mkutanao ya wakuu wa nchi na Serikali wa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) uliyopangwa kufanyika nchini mwezi Agosti 2019 

Kwa upande wa waheshimiwa Mabalozi hao walifurahishwa kwa hatua ya maandalizi iliyofikiwa, na kuelezea furaha yao kuhusu uwamuzi wa Serikali kuwashirikisha mapema katika maandalizi hayo.
Sehemu ya Mabalozi wa Nchi za Afrika na wanachama wa Jumuiya ya SADC wakimsikiliza Prof. Palamagamba John Kabudi (hayupo pichani) 
Sehemu nyingine ya watumishi judoka Balozi za Afrika zilizopo nchini 
Prof. Palamagamba John Kabudi akifafanua jambo kwa Waheshimiwa Mabalozi alipokutana nao 
Balozi wa Afrika Kusini akielezea jambo katika mkutano na Waziri Prof. Palamagamba John Kabudi 
Mkutano ukiendelea.

No comments: