Ibrahim Ajibu
AKIWA Rustenburg, Afrika Kusini kiungo mshambuliaji mpya wa Simba, Ibrahim Ajibu na Francis Kahata wamekiona cha moto ni baada ya Kocha Mbelgiji, Patrick Aussems kutumia saa mbili sawa na dakika 120 kuwakimbiza nyota hao.
Hiyo, ikiwa ni saa chache tangu timu hiyo itue Sauzi na kuweka kambi kwenye moja ya hoteli nyota tano ya Royal Marang Hotel ya nchini huko ikijiwinda na Ligi ya Mabingwa Afrika na Ligi Kuu Bara.
Ajibu alijiunga na Simba hivi karibuni akitokea Simba mara baada ya mkataba wake kumalizika wa kuichezea timu hiyo huku Kahata yeye amejiunga na timu hiyo baada ya mkataba kumalizika Gor Mahia ya nchini Kenya. Ibrahim Ajibu atakaa siku sita tu katika kambi yao ya Afrika Kusini kisha atarejea hapa na kujiunga na Taifa Stars.
Akizungumza na Spoti Xtra, Meneja wa timu hiyo Patrick Rweyemamu alisema mara baada ya kutua huko juzi Jumatatu walifanya program moja ya mazoezi ya jioni kwa kutoa uchovu wa safari lakini siku iliyofuata walifanya mara mbili asubuhi na jioni.
Rweyemamu alisema, programu waliyoanza nayo ya fi tinesi kwa ajili ya kuongeza pumzi na kasi ya ndani ya uwanja kuanza ya kimbinu ndani ya uwanja kwa lengo la kuweka utimamu wa mwili.
Aliongeza kuwa, mazoezi hayo yanahusisha mbio fupi na ndefu huku wakiruka koni ili kuhakikisha wanarejea katika viwango vyao baada ya kumaliza mapumziko.
“Kila mchezaji anaonekana kufanya mazoezi kwa nguvu huku wakifuata maelekezo kutoka kwa kocha wao wakiwemo wachezaji wapya waliosajiliwa,” alisema Rweyemamu.
Timu hiyo ikiwa kambini huko Sauzi imepanga kucheza michezo mitatu ya kimataifa ya kirafi ki dhidi ya Orlando Pirates ya nchini huko kabla ya kurejea nyumbani kuvaana na Enyimba kwenye Siku ya Simba. GPL
No comments:
Post a Comment