ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, August 15, 2019

RAIS CYRIL RAMAPHOSA WA AFRIKA KUSINI AWASILI NCHINI KWA ZIARA RASMI YA SIKU MBIL

Rais Cyril Ramaphosa na mkewe Dkt. Tshepo Motsepe wakiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo. 

RAIS wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa na mkewe, Dkt. Tshepo Motsepe, wamewasili nchini Tanzania usiku wa kuamkia leo na kupokelewa na mwenyeji wao, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba Kabundi ambaye alimwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli..
…Akilakiwa na Prof. Kabudi.

Ramaphosa amewasili kwa ziara rasmi ya siku mbili nchini kabla ya kuhudhuria Mkutano wa Viongozi Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) ambao utaanza keshokutwa Jumamosi, Agosti 17, 2019 jijini Dar es Salaam.
…Akiongozana na Prof. Kabudi.
…Akisalimiana na Mkuu wa Wilaya (DC) wa Ubungo, Kisare Makori. Wengine kutoka kushoto ni DC wa Kinondoni, Daniel Chongolo; DC wa Kigamboni, Sarah Msafiri na DC wa Ilala, Sophia Mjema.

….Akisalimiana na DC Mjema.


…Akisalimiana na RPC wa Kanda Maalum ya Dar es salaam, Lazaro Mambosasa.

No comments: