ANGALIA LIVE NEWS

Monday, August 26, 2019

TULIPOFIKIA MSIBA DMV

Kwanza tumshukuru Mwenyezi Mungu, pili Shukrani mno wana DMV na waTanzania wote USA kwa rambirambi zenu.

Shukrani nyingi kwa wale wote waliojumuika na kuleta vitu vya mnada na wote waliokuja na michango yao katika harambee iliyofanyika siku ya Jumapili na kuwezesha Kufanikisha harambee ya mpendwa mama yetu.

Fedha iliyopatikana kwenye harambee ni $3,100 na imewezasha kufikisha jumla ya makusanyo yote $14,100 tumebakiza $3,900 kufikia lengo

Tunawashukuru wote kwa ujumla wenu kwa michango na rambirambi zenu na kushikamana na wafiwa katika kipindi hiki kigumu.

Tunaomba bado nguvu yako tumalizie hiyo sehemu ya fedha iliyobaki ili iwezeshe kumpeleka mpendwa wetu Tanzania na hatimae kumpumzisha katika nyumba yake ya milele.

Tafadhali tuma rambirambi zako kupitia

CashApp au Zelle ya Mume wa Jackie, Andrew Tandau: 240-421-8392.
GoFundMe Account https://www.gofundme.com/f/celebration-of-life-mama-cecilia-korassa.

Tunatanguliza shukurani kwa mchango wako.

 Update kamili ya michango yote na Misa Jumamosi ifafuata baadae

Kwa maelezo zaidi piga:
240-462-2480 - Richard Mawenya
410-262-9812 - Pricilla Msaki
301-549-4019 - Doris Gao
240-393-8445 - Julius Manase

BWANA AMETOA, BWANA AMETWAA NA JINA LAKE LIHIMIDIWE.

No comments: