ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, September 28, 2019

DKT.MASSANGWA AONGOZA IBADA YA MAZISHI YA NELSONI ALIYEFARIKI KWA AJALI YA NDEGE

Jeneza lililobeba Mwili wa Marehemu Nelson Olotu likiwa kanisani tayari kwa Ibada ya Maziko.
Baadhi ya waombolezaji wakiwa katika ibada ya mazishi katika kanisa la KKKT Usharika wa Sasi mtaa wa Ilmeshorori,Dayosisi ya Kaskazini Kati 
Gari lioilobeba mwili wa Nelson likiondoka eneo la kanisa kuelekea makaburini kwaajili ya maziko.
Na Vero Ignatus, Arusha
ASKOFU wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Kati Dk.Solomon Masangwa ameongoza ibada ya mazishi ya aliyekuwa mwanafunzi wa Urubani Nelson Olotu (25) aliyefariki kwa ajali ya ndege Septemba 23, 2019.
Aidha katika ajali hiyo iliyotokea hivi karibuni kwenye kiwanja kidogo cha ndege kilichopo Seronera mbuga ya wanayama Serengeti Mkoani Mara, pia mtoto wa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania (CDF) Jenerali Venance Mabeyo, Nelson Mabeyo ambaye alikuwa rubani wa ndege hiyo namba 5H-AAM ya kampuni ya Auric Air naye alifariki dunia.
Akizungumza katika ibada hiyo Jumamosi Septemba 27, 2019 iliyofanyika katika Usharika wa Sasi mtaa wa Ilmeshorori, Dayosisi ya Kaskazini Kati,Dk.Masangwa aliwapa pole wazazi na ndugu wote walioguswa na msiba huo na kuwataka kuwa na utulivu katika kipindi hicho cha majonzi.
"Binadamu siku zetu za kuishi hapa duniani fupi na zimejaa dhiki,hivyo hakuna ambaye ajuaye siku wala saa ya kifo kitakapompata, kutokana na fumbo hili inatupasa kila mmoja kukesha tukiomba,"alisema
Alisema ajali za ndege zinasababishwa na mambo mbalimbali kuanzia inaporuka,ikiwa angani na inapotua hivyo ni suala la kumwachia mungu.
"Baadhi ya sababu hizo ni makosa ya rubani,matatizo ya kiufundi,hali ya hewa,vyuma,wakati wa ndege kupaa na wakati wa kutua,huweza kusababisha ajali katika hili hakuna wa kulaumiwa,"alisema
Aidha alisema katika mazingira hayo huwezi kumlaumu mtu yoyote sababu hata rubani akijitahidi kukwepa ajali lakini bado mazingira ya ajali yanaweza kuwepo.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro alitoa salamu za pole kwa niaba ya serikali na kusema kazi ya mungu haina makosa.
"Huyu Nelson angemaliza safari ya masomo yake angetusaidia sana Serikali na taifa,lakini makusudi ya mungu lazima yatumike na tumwachie yeye,"alisema
Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya,ametoa pole na kusema hakuna mwenye jibu kwanini mtu mwenye umri mdogo kama walivyo vijana hao waliofariki katika ajali hiyo na katika kipindi hiki ambacho wazazi wao walikuwa wakiwahitaji kuliko kipindi chochote.
"Mahali salama na pekee ni kujikabidhi mikononi mwa mungu,"alisema Katibu wa Chama cha Marubani nchini,Khalid Lqbal amesema marehemu alikuwa mpole,mnyenyekevu, msikivu ba mwenye kupanga kujifunza zaidi.
"Hivyo tumepoteza kijana mdogo ambaye angekuja kuwa msaada hapo baadaye,"alisema
Pia amesema vifo vya vijana hao Nelson Olotu na Nelson Mabeyo ni pigo kubwa kwa taifa na sekta ya masuala ya anga.
Kwa upande wa kaka wa marehemu aliyesoma histori fupi ya marehemu,Calvin Olotu alisema marehemu alisoma shule ya Msingi Trust St.Patrick mwaka 1998 na kumaliza 2009 na Sekondari ya Duluti ambayo alimaliza mwaka 2013.
Baada ya hapo alijiunga shule ya Urubani mwaka 2014 katika Chuo cha Aviation College Dar esalaam na kuhitimu mwaka 2015 kisha alikwenda kujiunga na Chuo cha urubani Nairobi nchini Kenya cha PRO-ACTIVE AVIATION COLLEGE na kuendelea na ground School na Flight mpaka mwaka 2019.
Calvin alisema marehemu alikuwa mtoto wa tatu katika familiya ya mzee Wilberd Phillemon Olotu na mauti yalipomkuta akiwa safarini katika Hifadhi ya Serengeti na amezikwa nyumbani kwa wazazi wake Kambi ya Chupa Wilaya ya Arusha.

No comments: