ANGALIA LIVE NEWS
Monday, October 14, 2019
LIVE: BABA WA TAIFA MWL NYERERE, RAIS MAGUFULI, MWENGE WA UHURU, VIJANA WAKUTANA LINDI
By Tumaini Msowoya, Mwananchi tmsowoya@mwananchi.co.tz
Dar es Salaam. Wanafunzi waliocheza halaiki katika kumbukumbu ya miaka 20 ya kifo cha mwalimu Julius Nyerere wamekuwa kivutio kwa kutengeneza maumbo ya ramani mbalimbali.
Maadhimisho hayo yanayofanyika sambamba na kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru katika uwanja wa Ilulu mkoani Lindi.
Wanafunzi hao wameunda maumbo ya ramani ya Tanzania, Mkoa wa Lindi, Mwenge wa Uhuru na Bendera ya Taifa pamoja na umbo la mjusi mkubwa wa Tanzania aliyepo nchini Ujerumani.
Rais wa Tanzania, John Magufuli ndio mgeni rasmi katika maadhimisho hayo.
‘Tumejitahidi, tunatekeleza, awamu ya tano 2015-2020,’ ni baadhi ya maneno yaliyoumbwa na wanafunzi hao.
Wanafunzi hao waliovaa mavazi meupe walitembea kama askari kuelekea mbele ya jukwaa wakiwa wameshika njiwa ambao baadaye waliwaachia na kuruka.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment