ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, October 31, 2019

Watuhumiwa wa Wizi wa Tausi wa Ikulu Wahukumiwa

JUMATANO Oktoba 30, 2019, watuhiwa watatu wa kesi ya wizi wa tausi ikulu wameachiliwa huru kwa masharti na Mahakama ya hakimu mkazi kisutu.

Akitoa hukumu hiyo Hakimu Mkazi Thomas Simba amesema, washtakiwa hao Washitakiwa hao ni David Graha, Mohammed Hatibu na Mohammed Ally wameachiliwa kwa masharti ya kulipa fidia ya Sh. Milion 6.8 kiasi ambacho ni mara mbili ya gharama ya nyara walizoziiba kutokana na kuisababishia hasara serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hakimu Simba amesema kuwa washtakiwa wote kwa pamoja hawatakiwi kufanya kosa lolote katika kipindi cha miezi 6 na kuamuru kutaifishwa kwa nyara hizo (Tausi) kwa serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Washitakiwa wanakabiliwa na mashitaka matano wanayodaiwa kuyatenda Juni Mosi 2015 na Oktoba 14, mwaka huu.

Anadaiwa katika mashitaka ya kujihusisha na mtandao wa uhalifu, katika tarehe hizo maeneo ya Dar es Salaam kwa pamoja waliratibu genge la uhalifu wakijihusisha na biashara ya ndege aina ya tausi bila kibali cha Mkurugenzi wa Wanyamapori.

Mashitaka ya pili, wanadaiwa katika tarehe hizo washitakiwa walikutwa na ndege watatu aina ya tausi wenye thamani ya Dola za Marekani 1,500 sawa na Sh milioni 3.4 mali ya serikali bila kuwa na kibali. GPL

No comments: