ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, November 17, 2019

MEYA SITA ASHAURI WANANCHI KUPENDA BIDHAA ZINAZO ZALISHWA NYUMBANI, ASEMA ZINAUBORA WA HALI YA JUU

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Mhe. Benjamini Sita wa pili kulia mwenye suti, akikagua bidhaa za ngozi zinazozalishwa na wajasiriamali wa Halmashauri hiyo. Wa kwanza kulia ni Mkuu wa Idara ya Mifugo na Uvuvi, Dk. Patricia Henjewele.
NA MWANDISHI WETU
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya kinondoni, Mhe. Benjamini Sita amesema kuwa kunahaja ya kuangalia namna ya kuwajengea uwezo wananchi kuwa natabia ya kununua bidhaa zinazozalishwa hapa nchini.

Meya Sita ametoa kauli hiyo leo, wakati akikagua mabanda ya maonesho ya wajasiriamali yaliyoandaliwa na Manispaa nakuwezeshwa na Mamlaka ya Biashara Tanzania Tan Tredi.
Meya sita amesema kuwa amefurahishwa na manispaa kuandaa maonesho hayo kwani kufanya hivyo ni njia mojawapo ya kuwatia moyo wajasiriamali na hivyo kupata fursa ya kutangaza bidhaa zao.
Amefafanua kuwa Tanzania inauwezo mkubwa wakuzalisha bidhaa zangozi zenye ubora kutoka kwa wajasiriamali wa ndani na hivyo itaondoa dhana ya watu kwenda kununua bidhaa hizo nje ya nchi.
“ Tanzania tunauwezo mkubwa wakuzalisha vitu vizuri,tunapaswa kushirikiana kwa pamoja ili tuhakikishe bidhaa zetu zinapata soko la kutosha , lazima tutengeneze mazingira ya wenzetu kupata miundombinu ya vifaa ili waweze kuzalisha bidhaa nyingi nakupata soko nje ya nchi.

Meya sita alishauri kuwepo kwa masoko ya kati ya bidhaa( Supermarket) ili kuwezesha wananchi kupata bidhaa hizo kwa urahisi pindi wanapokwenda kununua mahitaji mengine jambo ambalo litaweza kuleta uzalendo na hivyo kuitangaza nchi kimataifa kupitia bidhaa za ngozi.
Kwaupande wake Mkuu wa Idara ya Mifugo na Uvuvi,Dk. Patricia Henjewele alisema kuwa maonesho hayo yamekwenda sambamba na mafunzo ya utangazaji wa bidhaa ambapo wajasiriamali kutoka Manispaa ya Kinondoni wameshiriki.

Alifafanua kuwa baada ya kumalizika kwa maonesho hayo na mafunzo, halmashauri imeandaa maonesho mengine yatakayofanyika Disemba 12 hadi 15 katika viwanja vya Tanganyika Pekazi ambapo wajasiriamali kutoka sehemu mbalimbali watashiriki.
Kwaupande wao washiriki wa maonesho hayo wameipongeza manispaa ya Kinondoni kwakuandaa mafunzo hayo kwani imekuwa fursa kutangaza bidhaa ambazo wamezizalisha wenyewe na hivyo kuomba wananchi kuwaunga mkono.

No comments: