ANGALIA LIVE NEWS
Sunday, November 3, 2019
Rais Magufuli Amteua Charlse Kichele Kuwa CAG Mpya
Katibu Mkuu Kiongozi, John Kijazi
Katibu Mkuu Kiongozi ndugu John Kijazi leo Novemba 3 ametangaza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa Viongozi wa Nafasi mbalimbali kama ifuatavyo:-
1. Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) -amemteua Charles Edward Kichele kuanzia Nov 4, 2019 kuchukua nafasi ya Prof. Mussa J. Assad (CAG) ambaye kipindi chake cha uteuzi wa miaka mitano hiyo kinakwisha siku ya kesho. Kabla ya uteuzi huo Kichele alikuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe.
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) mpya, Charles Edward Kichele.
2. Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe ameteuliwa na Magufuli kuwa Katalina Tengia Levekati ambaye alikuwa Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania anachukua nafasi ya Kichele.
Magufuli Amemteua Mwandisi Aisha Amuru kuwa balozi wa Tanzania nchini Kuwait awali alikuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro.
Pia Magufuli amemteua Kamishina wa kazi Kanari Francis Leonard Mbindi kuwa Kamishina wa Kazi katika Ofisi ya Waziri Mkuu ili kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Gabriel Warata ambaye ameteuliwa kuwa Naibu Wakili Mkuu wa Serikali pamoja na majaji 12 wa Mahakama Kuu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment