ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, November 2, 2019

OFISI YA MAKAMU WA RAIS KWA KUSHIRIKIANA NA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA YAKUTANA NA WAZALISHAJI, WASAMBAZAJI NA WAUZAJI WA MIFUKO MBADALA WA PLASTIKI

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais, Bi Kemilembe Mutasa akiongea wakati wa Mkutano uliokutanisha Wazalishaji, wasambazaji na Wauzaji wa mifuko mbadala wa plastiki katika ukumbi wa JNICC jijini Dar Es Salaam. Kikao hiko kimeandaliwa kwa ushirikiano wa Ofisi ya Makamu wa Rais na Wizara ya Viwanda na Biashara.
Mgeni Rasmi katika katika kikao cha wazalishaji, wasambazaji na wauzaji wa mifuko mbadala wa plastiki, ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Viwanda toka Wizara ya Viwanda na Biashara Bwana Leo Lyayuka akifungua kikao hiko kilichofanyika katika ukumbi wa JNICC jijini Dar Es Salaam.
Mgeni Rasmi katika kikao cha wazalishaji, wasambazaji na Wauzaji wa mifuko mbadala kilichoandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais na Wizara ya Viwanda na Biashara Bwana Leo Lyayuka akiwa katika picha ya pamoja na Washiriki waliohudhuria kikao hiko katika Ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC)

Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kushirikiana na Wizara ya Viwanda na Biashara imeandaa kikao kilichowakutanisha Wazalishaji, Wauzaji na Wasambazaji wa mifuko mbadala wa plastiki. Kikao hiko kimefanyika katika Ukumbi wa Mwalimu Julius Kmbarage Nyerere (JNICC) jijini Dar Es Salaama

Lengo la Kikao hiko ni kusikiliza hoja na changamoto mbalimbali kutoka kwa Wazalishaji, Wauzaji na Wasambazaji wa mifuko hiyo, na hivyo basi kuwezesha Serikali kuzipatia changamoto hizo uvumbuzi.

Akiongea katika Kikao hiko Mgeni Rasmi ambaye ni Mkurugenzi wa Viwanda kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara Bw. Leo Lyayuka alisema kuwa zoezi zima la upigaji marufuku mifuko ya plastiki limefanikiwa kwa kiasi kikubwa na lilifanyika kwa weledi hali iliyopelekea kutokua na malalamiko yoyote kutoka kwa wananchi.

Kwenye mafanikio yoyote hapakosi changamoto, vivohivyo, kwenye zoezi hili, ingawa tumepata mafanikio makubwa lakini kuna changamoto ambazo zimejitokeza na kama zisipotafutiwa ufumbuzi wa haraka zitaharibu na kurudisha nyuma mafanikio makubwa yaliyopatikana. Kwahiyo kikao chetu kitajikita katika kuzibaini changamoto zote na kupendekeza mapendekezo namna ya kutatua alisema Bwana Lyayuka.

Naye Mkurugenzi Msaidizi toka Ofisi ya Makamu wa Rais Bi Kemilembe Mutasa alisema kuwa Kikao hiko kina lengo la kujenga uelewa wa pamoja kuhusu utekelezaji wa katazo la mifuko ya plastiki, kuibua changamoto za utekelezaji na namna ya kukabiliana na changamoto husika hususani katika masuala yafuatayo:- Viwango vya ubora vinavyotakiwa vya mifuko mbadala wa plastiki, Hali ya uzalishaji na usambazaji wa mifuko mbadala wa plastiki, Uzalishaji na upatikanaji wa malighafi kwa ajili ya mifuko mbadala wa plastiki, Viwango vya ubora wa mifuko mbadala na Changamoto zinazojitokeza katika uzalishaji wa mifuko mbadala wa plastiki.


Ofisi ya Makamu wa Rais imekua ikiandaa vikao kama hivyo mara nyingi ili kuweza kupata maoni na changamoto juu ya uzalishaji, usambazaji na biashara ya mifuko mbadala wa plastiki kwa pamoja.


No comments: