ANGALIA LIVE NEWS

Friday, November 1, 2019

RC DKT. REHEMA NCHIMBI AKABIDHI GARI KIKOSI CHA ZIMA MOTO NA UOKOAJI MKOA WA SINGIDA

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi akipeana mkono na Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoani hapa, Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACF), Ivo Ombella wakati akikabidhi gari aina ya‘Land Lover Defender’ kwa Jeshi hilo katika hafla iliyofanyika jana. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Singida, Mhandisi Paskasi Muragili.
Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Singida, Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACF), Ivo Ombella akizunguza baada ya kukabidhiwa gari hilo.
Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Singida, Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACF), Ivo Ombella (wa pili kulia) akiwa na maofisa wa jeshi hilo katika hafla ya kukabidhiwa gari hilo.
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi, akiwa na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa mkoa huo katika hafla ya kukabidhi gari hilo.
Gari aina ya ‘Land Lover Defender’ lililokabidhiwa kwa Jeshi la Zima moto na Uokoji mkoani hapa.

Na Dotto Mwaibale, Singida

MKUU wa Mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi amewataka wananchi kujiepusha na majanga ya moto yanayotokana na uzembe au makusudi kwa kigezo cha kutegemea uwepo wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.

Dkt. Nchimbi aliyasema hayo jana wakati akikabidhi gari aina ya‘Land Lover Defender’kwa Jeshi la Zima moto na Uokoji mkoani hapa litakalotumika kwa shughuli mbalimbali za utawala.

“Natarajia gari hili liitasaidia kurahisisha majukumu ya kijeshi kwa Jeshi hili, hususan kwenye eneo la utoaji elimu na kujenga maarifa kwa jamii katika kuhakikisha suala la kinga linapewa kipaumbele ili kuepusha maafa na ajali zozote huko mbeleni,” alisema Nchimbi.

Kwa upande wake, Kamanda wa Jeshi hilo mkoani hapa, Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACF), Ivo Ombella, alisema gari hilo litatumika kwa shughuli zote za dharula ndani ya jeshi hilo chini ya uratibu wa idaraya utawala.

“Ifahamike kuwa Jeshi la Zima moto na Uokoaji linahusika nadharula zote ikiwemo majanga ya moto, tetemeko la ardhi, mafuriko na uzazi isipokuwa jinai pekee,” alisema Ombella

Aidha, aliwatahadharisha wananchi kuwa makini kwa kujiepusha na majanga ya moto hasa nyakati za utayarishaji wa mashamba kwa kuzingatia usalama na utunzaji mzuri wa mazingira kulingana na eneo husika.

No comments: