Advertisements

Wednesday, January 8, 2020

Diamond Platnumz apiga shoo ya kibabe CAF wimbo wa Yope wampagawisha Sadio Mane, Eto’o

Mwanaspoti-Tuzo CAF-Yope ya Diamond Platnumz-Sadio Mane-Eto’o-Tanzania-muziki
By Eliya Solomon

Dar es Salaam. Mwanamuzi Diamond Platnumz alinogesha usiku wa sherehe za tuzo za soka Afrika zilizofanyika Hurghurda nchini Misri na kushuhudiwa Sadio Mane akitwaa tuzo.

Diamond anatumbuiza kwa mara ya pili katika tuzo hizo aliwapagawisha wageni waliofika katika ukumbi huo wakiongozwa huku Samuel Eto’o na Sadio Mane wakishindwa kujizuia na kwa kucheza wimbo wa Yope.

Katika tuzo hizo mshambuliaji wa Mane alitangazwa usiku wa Jumanne kuwa mwanasoka bora wa Afrika kwa mwaka 2019 baada ya kuisaida klabu yake ya Liverpool kutwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya huku akiliongoza pia taifa lake la Senegal kufika fainali ya mataifa Afrika 'Afcon'.

Mane, 27, ametwaa tuzo hiyo kwa mara yake ya kwanza baada ya kumaliza katika nafasi ya pili katika miaka miwili mfululizo, 2017 na 2018, nyuma ya mchezaji mwenzake wa Liverpool, Mohamed Salah. Mwaka 2016 alishika nafasi ya tatu.


Nyota huyo, amekuwa mchezaji wa pili katika historia ya taifa Senegal kutwaa tuzo hiyo kubwa Afrika baada ya El Hadji Diouf, ambaye alifanya hivyo katika miaka ya 2001 na 2002.

Baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo, Mane alisema,"Mpira ni kazi yangu, ninayoipenda sana, ninafuraha kushinda tuzo hii. Nichukue fursa hii kuwashukuru watu wote wa Senegal, wamekuwa wakisukuma hatua zangu.ADVERTISEMENT

"Pia napaswa kutoa shukrani zangu za dhati kwa kocha wangu wa (Senegal), Aliou Cisse na wa Liverpool (Klopp) pamoja na wachezaji wenzangu."

Salah hakuonekana katika usiku huo wa sherehe za tuzo za Afrika na badala yake alikuwa na kikosi chake cha Liverpool ambacho kilikuwa na program ya mazoezi kwenye uwanja wa Melwood.

Zipo ripori zinazosema kutohudhuria kwa Salah katika sherehe hizo ni kutokana na mgogoro uliopo na shirikisho la soka nchini humo. Kama angetwaa Salah tuzo hiyo, inamaana angekuwa mchezaji wa tatu kutwaa tuzo hiyo mara tatu.

Mane ametwaa tuzo hiyo, kufuatia kupigiwa kura na makocha wa timu za Taifa, wakurugenzi wa ufundi na manahodha ambao mataifa yao ni wanachama wa shirikisho la soka Afrika, CAF.

Tuzo nyingine zilienda kwa Achraf Hakimi,ambaye anaichezea Borussia Dortmund kwa mkopo akitokea Real Madrid, amekuwa chipukizi bora wa mwaka.

Aliyeibuka kuwa kocha bora wa mwaka ni Djamel Belmadi baada ya kuiongoza Algeria kubeba ubingwa wa Afcon

Kikosi bora cha Afrika kwa mwaka 2019 : Andre Onana; Serge Aurier, Joel Matip, Kalidou Koulibaly, Achraf Hakimi; Idrissa Gana Gueye, Riyad Mahrez, Hakim Ziyech; Mohamed Salah, Pierre Emerick Aubameyang, Sadio Mane

TUZO NYINGINE 2019

Mchezaji bora wa mwaka wa ndani: Youcef Belaïli (Algeria & Esperance / Ahli Jeddah)

Timu bora ya mwaka kwa wanawake : Cameroon

Timu bora kwa wanaume ya mwaka: Algeria

Goli bora la mwaka : Riyad Mahrez (Algeria)

Kocha bora wa kike wa mwaka: Desiree Ellis (South Africa)

Rais bora wa klabu Afrika: Moise Katumbi (TP Mazembe)

Mchezaji bora wa kike Afrika : Asisat Oshoala (Nigeria & Barcelona)



No comments: